MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe amesema chama chake kitazuia bajeti
ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa
mkutano wa Bunge la Bajeti unachotarajiwa kuanza Juni 12.
Mbowe
alisema kuwa watafanya hivyo hadi Serikali itakapotoa ufafanuzi kuhusu
hatima ya wakazi wa Tandahimba waliochomewa mali zao wakati wakiandamana
kuadai haki zao akieleza kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu ni suala
lisilokubalika.
Alitoa kauli hiyo alipohutubia mkutano wa hadhara
uliofanyika Tarafa ya Mahuta wilayani Tandahimba mkoani Mtwara ambapo
alidai kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na Serikali ya CCM ndivyo
vilivyoisukuma Chadema kufanya oparesheni nchi nzima na kwamba lengo la
chama chake ni kuchukua dola katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
“Hili
la korosho na vurugu zilizotokea hatuwezi kuliacha hivi hivi, Chadema
tutazuia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Wizara ya
Mambo ya Ndani, hadi hapo Serikali itakapotoa tamko la hatima ya watu
waliochomewa mali zao. Tunataka polisi watueleze wale waliojihusisha na
vitendo hivyo wapo wapi na wanafanywa nini?”alisema Mbowe akihoji..
Alisema
kuanzia sasa chama hicho kitahakikisha waathirika wote wa vurugu
zilizofanyika mwezi Aprili mwaka huu, wanalipwa fidia na Serikali kwa
kuwa utafiti waliofanya unaonyesha kuwa vurugu hizo zilisababishwa na
kufanywa na polisi.
“Serikali lazima itoea tamko, hatua gani
wamechukuliwa watu waliochoma maduka ya wananchi na mali zao. Chadema
haiwezi kukubali na mimi niko tayari kufunguliwa kesi zaidi za uchochezi
na hata kufungwa jela, lakini sitaacha kuelimashi wananchi juu ya haki
zao na ninawamba muunge mkono Chadema ichukue dola mwaka 2015 ili mpate
ukombozi wa kweli,”alisema.
Mbowe ametoa msimamo huo wa chama
ikiwa ni muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa
kueleza dhamira ya chama hicho kuwa ni kuhakikisha inawatetea kwa nguvu
zote wakazi wa Tandahimba walioharibiwa mali zao na kwamba chama hicho
kimemkabidhi jukumu hilo Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni .
Mbowe
alisema Chadema hakipo kwa ajili ya kuwania udiwani na uenyekiti wa
serikali za mitaa bali ni kuingia Ikulu kuongoza dola na kuleta utetezi
wa kweli wa rasimali za watanznaia zikiwamo madini gesi na mafuta
kuwanufaisha pia wakazi wa maeneo zinakotoka.
Alisema dhamira ya
Chadema ni kuondoa serikali ya CCM katika uchaguzi wa 2015 na kuwataka
wakazi wa mikoa ya kusini kutuyumbishwa na propaganda za udini,ukabila
ukanda na kuwataka wakazi wote wa kusini kuchagua chama chenye mlengo wa
kuwakomboa bila kujali ni chama gani.“Hadi sasa mimi ninakesi tisa za uchochezi, sitanyamaza hata
wakiniongezea nyingine, nitaendelea kusema ukweli kuhusu masuala ya
ukombozi wa wananchi,wakitika wanifunge na hata nikifa wakati wa
mapambano wanamageuzi wote wekeni maiti yangu pembeni songeni
mbele,ukombozi utaletwa na wanawake na wanaume, ”alisemaMbowe.
Akizungumzia
utitiri wa vyama vya siasa nchini alisema hiyo ni mbinu za CCM za
kudhoofisha upinzani ambapo wanatumia mbinu ya wagawe watatawenye
iliyotumiwa na wakoloni walipotawala bara la Afrika.