MENU

Thursday, June 7, 2012

Real Madrid yamshika Ronaldo

MADRID,Hispania
WINGA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema hafikirii kuondoka klabu hiyo ya Hispania na badala yake angependa kuona anamaliza jukumu la kucheza soka hapo hasa baada ya kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania.
Ronaldo (27), aliyeweka rekodi ya uhamisho ya pauni 80 milioni (Sh191 bilioni) akitoka klabu ya Manchester United ya England, amefunga mabao 46 ligi kuu msimu uliopita na kumaliza utawala wa Barcelona uliodumu kwa miaka minne.
"Kama uamuzi ungekuwa wangu, basi ningependa kubaki Real Madrid mpaka nitakapostaafu soka, ni kweli kabisa," alisema Ronaldo."Leo hii ningekuwa tayari hata kusaini miaka 10 kubaki hapa, lakini uamuzi kama huu unategemea pia watu wengine."
Ronaldo, aliyefunga mabao 55 katika mechi 60 za mashindano msimu uliopita, alikiri kwamba ana hamu ya kurejesha kile alichofanyiwa na klabu hiyo kwa kumpa dau kubwa la uhamisho.Aliongeza: "Yote niliyofanya, nimefanya kwa jasho langu na kipaji, lakini hakuna litakalopotea angani."Kwa sasa naendelea kubaki mchezaji niliyehamishwa kwa ada kubwa, na siku zote nimekuwa nikijaribu kuthibitisha hilo uwanjani," alisema.
Ronaldo, ni sehemu ya kikosi cha Ureno kinachojiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya na amefurahishwa kuona kocha wake, Jose Mourinho amesaini mkataba tena na Madrid mpaka mwaka 2016.
Katika mahojiano na gazeti la Hispania, Marca, alisema: "Nimefurahi kuona Mourinho akibaki.
"Klabu kama Real Madrid inapaswa kuwa na kocha mzuri kama [Jose]Mourinho.Kocha ameamua kubaki, na kwangu naamini Real Madrid haiwezi kutwaa Kombe bila Mourinho kuliko kama angekuwapo kwenye benchi."