MENU

Tuesday, June 26, 2012

Diamond, Shetta wang'ara Tamasha la Wajanja Moro


 

 Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Diamond na Shetta walikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wakati walipotumbuiza kwenye onyesho la 'Tamsha la Wajanja' lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Nyota hao waliibua shangwe na nderemo kubwa kutoka kwa mashabiki baada ya kupanda jukwaani na kuimba kwa kupokezana wimbo walioshirikiana uitwao 'Nidanganye'.
Mbali na Diamond na Shetta, wengine walioshangiliwa sana na mashabiki ni pamoja na Fid Q na Ommy Dimpoz aliyechengua kwa nimbo zake za 'Baadaye' na 'Nai Nai'.
Mkuu wa kitengo cha mahusiano na mawasiliano cha kampuni ya huduma za simu ya Vodacom ambao ndio waandaaji wa onyesho hilo, Joyclyine Kamuhanda, alisema kuwa onyesho hilo limelenga kuwaweka pamoja Watanzania na pia kuwawezesha kuwashuhudia wanamuziki hao waliowachagua.
Aliongeza kuwa baada ya onyesho hilo kufanyika Dar Es Salaam na Morogoro, wanatarajia kwenda katika mikoa mingine kama Tanga (Julai Mosi) na Mtwara ambako watafanya onyesho hilo Julai 8.