MENU

Friday, June 29, 2012

Ulimboka ana siri nzito

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Steven Ulimboka, akiwa amelazwa katika Chumba maalum cha wagonjwa mahututi (ICU)akiendelea na matibabu katika Taasisi ya mifupa (MOI)jijini Dar es Salaam jana.
ASEMA ATAANIKA KILA KITU BAADAYE, ASEMA ACHWE APUMZIKE, MKUU WA JOPO LA MADAKTARI WANAOMTIBU ASEMA ALING'OLEWA KUCHA, MENO MAWILI NA KUPATA MTIKISIKO WA UBONGO 

 MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari aliyetekwa nyara na kuumizwa vibaya  usiku wa kumkia juzi, kisha kutupwa  Msitu wa Pande, Dk Steven Ulimboka amesema atazungumza kwa kina yote yaliyomsibu baadaye na kuomba sasa aachwe auguze maumivu makali yanayomkabili.

Dk Ulimboka aliokotwa na wasamaria wema juzi asubuhi katika Msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kutekwa nyara na watu waliokuwa na silaha akiwa katika Viwanja vya Klabu ya Leaders, Kinondoni.

Jana, Dk Ulimboka ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili huku hali yake ikiwa haijatengemaa vyema, alitoa kauli akisema ingawa ana maumivu makali anaendelea vizuri ikilinganishwa na siku ya kwanza.

Dk Ulimboka alitoa kauli hiyo baada ya kutakiwa aeleze mkasa huo uliomfika wa kukamatwa, kuteswa na kutupwa msituni.



Hata hivyo, hadi sasa wingu zito la nani alimteka na watekaji walitaka kujua nini kutoka kwa kiongozi huyo wa madaktari, bado limetanda.

Siri nzito
Akisimulia mkasa huo kupitia Kituo cha Redio cha Clouds FM, Dk Ulimboka alisema, akiwa katika klabu hiyo ya Leaders alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alikuwa atokee Tandika na baada ya kumsubiri ndipo alipofika kwenye klabu hiyo, lakini, alianza kujisikia vibaya tofauti na siku nyingine na kuongeza;  "Yaani  sikuwa na amani."

Alisema, "Mara, katikati ya maongezi tukaona mtu anaongea na simu. Ghafla tukiwa tunasema tuagane, wakaja watu kama watano hivi na bunduki, wakasema wewe na yule bwana mko free (huru), tunakuchukua wewe (Dk Ulimboka)," alieleza na kuongeza:

"Sijakaa sawa, nikaona nimeshaburutwa nikaanguka kwenye lami, wakaniinua na kuniingiza kwenye gari nyeusi, lakini halikuwa na namba."

Hata hivyo, jana Dk Ulimboka hakuonana na mwandishi wa habari hii, badala yake alirekodiwa, na Mwananchi kupata sauti yake  akijibu swali kuhusu hali yake na tukio hilo,  baada ya uongozi wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kuzuia watu kumwona.

Daktari huyo wa magonjwa ya binadamu, amelazwa katika chumba cha Wagonjwa Wanaohitaji Uangalizi Maalumu (ICU).

"Kidogo najisikia nafuu ikilinganishwa na nilivyokuja ingawaje, bado nina maumivu makali. Kwa hivyo, ingependeza niendelee na mapumziko na mtu yeyote anayetaka kuniona pengine hilo jambo lisifanyike sasa. Hivi sasa ni vizuri nipumzike," ilisikika sauti hiyo ya Dk Ulimboka.

Lakini, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wodini alikolazwa Dk Ulimboka, kuna ulinzi mkali wa madaktari na hairuhusiwi watu kumwona kiholela siyo tu kwa sababu za kutaka aachwe apumzike, bali pia kutowaamini watu ovyo.

Madaktari wanaolinda eneo hilo walisikika jana wakisema, “Huyu tunamlinda wenyewe na haiwezekani mtu asiyefahamika kuingia humu ndani, na hilo tutahakikisha sisi wenyewe,”alisikika akisema mmoja wa madaktari hao.

Kiongozi jopo la madaktari

Katika hatua nyingine, kiongozi wa jopo la madaktari wanaomuhudumia Dk Ulimboka, Profesa Joseph Kahamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa Dk Ulimboka ana majeraha mwili mzima.

“Ingawa kwa sasa anaendelea vizuri, Dk Ulimboka  ameumia sana, kwani mwili wake mzima una majeraha kutokana na kupigwa na watekaji hao,”alisema Profesa Kahamba na kuongeza:

“Aliumia mbavuni,kifuani, miguuni, mikononi ambako aling’olewa baadhi ya kucha za vidole na kichwani  na kinywani, ambako aling’olewa meno mawili,”alisema.

Alifafanua kwamba, kutokana na maumivu hayo ya kichwa, Dk Ulimboka alipata tatizo la mtikisiko wa ubongo, lakini akasisitiza kuwa madaktari bingwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha yake.

Uongozi wa Moi watoa neno

Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (Moi) umeeleza kuwa hali yake inaendelea vizuri ingawa bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha taasisi hiyo.

Msemaji wa Moi, Almas Jumaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa licha ya hali yake kuendelea vizuri, lakini  haingewezekana kwa waandishi wa habari kuingia ndani ya chumba alikolazwa na kumwona Dk Ulimboka.

“Mgonjwa anaendelea vizuri ukilinganisha na jana (juzi), anaongea, anawatambua watu wanaokwenda kumwona, lakini utaratibu wa kwenda kumwona kwa ninyi imeshindikana kwa sababu yupo (ICU) ni chumba chenye utaratibu wake,”alisema Jumaa.

Jumaa aliongeza kwamba ili mtu aweze kuingia wodini   analazimika kuvaa vazi maalumu na mavazi yaliyopo, yasingetosha, lakini pia wapo watu wanaoendelea kumpatia huduma ya matibabu.

Tamko la Jumuiya ya Madaktari

Wakati hali ya Dk Ulimboka ikiwa hivyo, madaktari wameipinga tume ya uchunguzi iliyoundwa na Jeshi la Polisi kuchunguza suala hilo, wakidai mazingira ya tukio hayaliondoi jeshi hilo kuhusika.

Katibu wa Jumuiya hiyo, Dk Edwin Chitage aliwaambia waandishi wa habari kuwa wangependa kuundwa kwa tume huru itakayofanya kazi ya kuchunguza tukio hilo na kutoa taarifa kwa umma.

“Madaktari kwa ujumla wetu tunalaani tukio la kutekwa nyara,kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Pande, lakini pia hatuna imani na tume iliyoundwa na Jeshi la Polisi kwa sababu mazingira ya tukio hayaondoi kuhusika ama kutohusika kwa jeshi hilo,”alisema Dk Chitage.

Chitage alitoa msimamo wa madaktari kuwa ni kuendelea na mgomo, huku akionya Serikali kuacha vitendo vya kuwatisha, kwa madai kuwa vitendo hivyo haviwezi kuwa suluhu ya mgogoro kati ya pande hizo mbili.

“Kumekuwa na vitisho kwa madaktari katika maeneo mbalimbali nchini, hususan Dodoma, Mbeya, Arusha na Mwanza. Tunaionya Serikali kuacha mara moja na itambue kuwa mgogoro huo hauwezi kumalizwa kwa namna nyingine yoyote bali ni kwa Serikali kutekeleza madai ya madaktari,”alisema Chitega na kuongeza:

“Sisi madaktari kwa umoja wetu, tumechoka kushuhudia Watanzania wakipoteza maisha kwa magonjwa tunayoweza kuyatibu, kufanya kazi katika mazingira magumu huku kukiwa hakuna mipango ya kuboresha mazingira ya kazi, kukosekana kwa dawa na vifaa tiba.”

Mgomo huo wa madaktari leo unaingia siku ya saba tangu ulipotangazwa na mwenyekiti huyo kuwa, ungeanza rasmi Jumamosi iliyopita.

EBSS kutua Lindi kesho


 

Jaji Mkuu wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search (EBSS) 2012, Ritha Paulsen amewataka wakazi wa mkoa wa Lindi wenye uwezo wa kuimba kujitokeza kwa wingi kesho katika ukumbi wa Police Officers Mess ili kupata nafasi ya kuwakilisha mkoa huo kwenye shindano hilo.

Ritha aliyekuwa akizungumzia usaili wa EBSS 2012 kwa mkoa wa Lindi alisema kuwa anatambua kuwa mkoa wa Lindi una vijana wengi na wenye vipaji vya kuimba, na ndio maana kwa mara ya kwanza mwaka huu EBSS itaufikia mkoa huo.

"Tangu shindano hilo lianze miaka sita iliyopita, mwaka huu ndio tumelifikisha mkoa wa Lindi, ili kuhakikisha tunapata vipaji kutoka karibu kila kona ya nchi hii," alisisitiza Ritha.

Shindano hilo lilianzia mkoa wa Dodoma halafu likaelekea visiwani Zanzibar ambako kote walipata wawakilishi watano watano wenye vipaji vikubwa ambavyo alisema ana hakika vitaleta ushindani mkubwa mwaka huu.

"Mimi binafsi nimeshangazwa na uwezo wa hawa vijana wa kuimba na kumiliki eneo la kuimbia na nashindwa kuelewa walikuwa wapi muda wote huu, yani nikisema kuwa EBSS mwaka huu ni moto inaamisha kuwa itakuwa na ushindani mkubwa kweli kweli," alisema Ritha.

Alisema kwa kuwa mwaka huu EBSS inatoa fursa kwa washiriki wa umri kuanzia miaka 16, bado wanaangalia vipaji vya washiriki katika umri huo kwa kuwa bado hawajawapata.

Shindano hilo mwaka huu linadhaminiwa na kampuni ya huduma za simu za mikononi ya Zantel, ambao watatoa Sh. milioni 50 kwa mshindi na mkataba wa kurekodi.

Dk. Mukangara apata ajali


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara amepata ajali ya gari leo mchana baada ya kuchomekewa na basi katika eneo la Nzega, Mkoani Tabora.

Wednesday, June 27, 2012

Wahamiaji 42 wafa kwenye lori Tanzania


 Tanzania
Wahamiaji haramu arobaini na wawili wamepatikana wakiwa wamekufa ndani ya lori walimokuwa wakisafiria katika mkoa wa Dodoma, nchini Tanzania.
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania, Pereira Silima, amesema kuwa watu hao waliokuwa wamesongamana ndani ya lori waliaga dunia kutokana ukosefu wa hewa safi.
''Taarifa tuliyopata ni kwamba kulikuwa na wasafiri waliokuwa wakisafirishwa kwenye lori, ambalo lilikuwa kama kontena na halikuwa na hewa ya kutosha''.Bwana Silima ameambia BBC.

wahamiaji walikuwa wanatoka Ethiopia

Amesema wahamiaji hao haramu kutoka Ethiopia walikuwa wakijaribu kuingia Malawi.
Kulingana na bwana Silima wahamiaji hao walianza kufariki dunia wakiwa safarini. Jihudi za wahamiaji hao kumjulisha dereva kuhusiana na hali yao hazikufanikiwa, na hivyo kusababisha maafa ya watu arobaini na moja ndani ya lori hilo.
Kulingana na naibu waziri huyo wa mambo ya ndani tukio hilo lilifanyika Jumatatu usiku. Na baada ya dereva huyo kugundua kuwa watu wamefariki, aliondoa miili yao na kuitupa nje kabla ya kutoweka.
Mtu mmoja alifariki dunia akifanyiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Dodoma.

uhamiaji haramu umeenea

Polisi nchini Tanzania wamesema wanamsaka dereva huyo ambaye alitoroka punde tu baada ya kushusha miili ya wahamiaji hao haramu.
Biashara ya kuwasafirisha wahamiaji haramu hasa wanaotoka nchi za Somalia na Ethiopia kupitia Tanzania imeenea sana. Wengi huelekea mataifa ya kusini mwa Africa kutafuta maisha bora.

Tuesday, June 26, 2012

Rich Revealed: Record Year For Billionaires

 Carlos Slim, Bill Gates and Warren Buffett
Mexican telecoms tycoon Carlos Slim has been named the world's richest person for the third year in a row with a fortune estimated at $69bn (£43.8bn).
Microsoft co-founder and philanthropist Bill Gates, 56, held on to second spot with a net worth of $61bn (£38.77bn) in Forbes' 25th anniversary issue of its world billionaire rankings.
He was followed by US investment guru and head of the Berkshire Hathaway conglomerate Warren Buffett, 81, with a net worth of $44bn (£27.96bn).
A record 1,226 billionaires made the list this year, up from 1,210 in 2011, with an average net worth of $3.7bn (£2.35bn).
They came from 58 countries, with most hailing from the US, followed by the Asia-Pacific region, Europe, the Americas and the Middle East and Africa.
There was plenty of movement on the list, with 128 billionaires entering for the first time and 117 dropping off.

Facebook co-founder Mark Zuckerberg, 27, continued his rise up the ranks with a net worth of $17.5bn (£11.12bn), making him the 35th richest person in the world.
Last month, the social networking site filed paperwork to become a public company, seeking to raise $5bn (£3.1bn) in the largest floatation ever by an internet company on Wall Street.
The most notable people to leave this year's list were Harry Potter author JK Rowling and Jim Balsillie, former co-chief executive of Research in Motion, the maker of BlackBerry.

The first British billionaire listed is at number 78 - the Duke of Westminster, Gerald Grosvenor, one of the UK's biggest landowners.
Virgin boss Richard Branson, industrial design innovator James Dyson and high street retail tycoon Philip Green and his wife Cristina came in at number 255, each with a fortune of $4.2bn (£2.66bn).

HII NDO ORODHA YA MATAJIRI WAKUBWA TANZANIA AZAM AONGOZA,MENGI PIA YUMO

  1. Said Salim Bakhressa: AZAM - Grain milling, corporate finance, passenger sea transportation, plastic packaging, marketing, polypropylene bags, other branches of engineering field, food industry, drinking water
  2. Aziz Abood: Abood buses,factories,truck company,tv&radio,properties)
  3. Nasoro: Doll trailers, superstar buses, royal buses, major shareholder-mtibwa sugar,kagera sugar, city water, truck company, properties
  4. Mohamed Dewji: Mohamed enterprises, factories, properties
  5. Rostam Aziz: Caspian; Vodacom
  6. Reginald Mengi: The IPP Group, Financial Consulting firm (IPP Consulting), Coca-Cola (Coca-Cola Kwanza, Bonite Bottlers and Kilimanjaro Spring Water), (IPP Bodycare Ltd (IPP Media). These include The Guardian Ltd; Nipashe, Alasiri, Kasheshe, Independent Television Ltd. (ITV), East Africa Television (EATV, formerly Channel 5)), Radio ONE, Sky-FM (in a joint venture with BBC) and East Africa Radio.
  7. Michael Ngaleko: Presicion Air Ltd
  8. Fidahussein: Africarriers,properties including heidary plaza, raha towers, zahra towers etc
  9. Yusuph Manji: Quality Group; Properties, Trucks
  10. Andrew Chenge: Worth US$ 1million (over 1 billion Tanzania shillings) in an overseas offshore account........unaweza pia ukaongeza list yako just email erickmatiko@gmail.com

Je tunajua nini kuhusu Freemasons?


 


Nanukuu ‘Freemasons wa Tanzania? Waliojitokeza waziwazi na kujitambulisha ni kina Chande “Andy Chande” ambao ni matajiri wafanyabiashara maarufu. Katika mahojiano aliyofanya na mwandishi Muhiddin Michuzi wa gazeti la Sunday News la tarehe 3 April 2005, Sir Andy Chande alikiri kuwa anao wanachama zaidi ya 3,000 (yeye mwenyewe ni District Grand Master), na kuwa wamekuwa wakishirikiana na Rais Yoweri Museveni, Makamu wa Rais wa Kenya Moody Awori, na Rais Mstaafu Ben Mkapa (hakutaka kutamka wazi kuwa ni wanachama, lakini wapo watu wengine wanaofahamu kuwa hao aliowataja ni wanachama wa hiyo kitu, pamoja na Mzee Mengi). Alitamka kuwa mtu yeyote akishajiunga na freemasonry hawezi kutoka tena, kwa maneno yake “Once a freemason, always a freemason”.

Tazama jibu la Sir Andy Chande alipoulizwa na Muhiddin Michuzi kuhusu yalipo makao makuu ya Freemasons nchini Tanzania: “It is located along Sokoine Drive, just behind the Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam. We have a licence to sell drinks to members; we have also been exempted by the government of Tanzania from registration We have the full blessings of the government. Once that building was about to be taken over for public purpose, but when I sent a memorandum to the State House, we got it back. You know, Mwalimu Julius Nyerere was not a Freemason, but he knew what Freemasonry is”.


DIAMOND AKIWA KATIKA POZI TOFAUTI


Diamond, Jaydee, Ali Kiba wang'aa Usiku wa Hollywood



Wasanii Diamond Platnumz, Lady Jaydee na Ali Kiba waliacha gumzo mwishoni mwa wiki wakati walipotumbuiza katika hafla maalum iitwayo Club E Hollywood Glam Night iliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza.Katika hafla hiyo ambayo ukumbi ulipambwa kwa mandhari kama ya Hollywood ya Marekani, wanachama wa Club E na wageni wengine waalikwa walipata burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii hao wa Kitanzania. Wasanii wote waliotumbuiza walivaa kama wasanii wa Hollywood na pia kulikuwa na picha mbalimbali wasanii nyota wa Hollywood na michezo mbalimbali ambayo ilichangamsha mandhari hayo. Kulikuwa pia na sehemu za kupiga picha na mavazi kama yanayovaliwa Hollywood, gurudumu la bahati yaani ‘wheel of fortune’ na pia wageni waalikwa walipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali. Msanii wa kwanza kupanda jukwaani alikuwa Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee ambaye aliimba nyimbo saba mfulululizo na bendi yake ya Machozi kabla hajapanda Ali Kiba. Wakati Kiba akiwa jukwaani, Jaydee alipanda tena na wakafanya onyesho la pamoja kwa kuimba wimbo wa Kiba wa ‘Single Boy, Single Girl’ huku mashabiki wakishangilia jinsi wasanii hao walivyotumia vipaji vyao vizuri. Yoyote aliyeona jinsi wasanii walivyovalia hakushindwa kugundua kwamba ulikuwa ni Usiku wa Hollywood ndani ya Jiji la Dar es Salaam. Ukumbini pia kulikuwa na picha za wacheza filamu maarufu kama Denzel Washington, Will Smith, Samuel L Jackon na Angelina Jolie. Makundi mawili ya dansi yenye vijana wenye vipaji, Best Friends na FBI hayakuachwa nyuma kwani vijana hao walitoa burudani ya aina yake na kuwafanya mashabiki kutaka zaidi. Naye msanii Diamond Platnumz hakuwaangusha mashabiki wake kwani alipopanda jukwaani aliwasha moto mwanzo hadi mwisho kwa nyimbo na uchezaji wake pamoja na madansa wake huku mashabiki pia wakiimba na kucheza. Baadhi ya watu waliohudhuria, waliwapongeza waandaaji wa hafla hiyo ya aina yake hasa kwa kuthamini wasanii wa ndani ambao walitoa burudani ya aina yake bila kusahau chakula chenye ubora wa hali ya juu ambacho kilipatikana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa shughuli. Club E, iliyoanzishwa mwaka 2007 na ina wanachama zaidi ya 2000 kote nchini, huandaa shughuli mbalimbali za burudani hususan kwa wanachama wake na wageni waalikwa kila mwaka.

DIAMOND THE SUPERSTAR

Diamond, Shetta wang'ara Tamasha la Wajanja Moro


 

 Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya, Diamond na Shetta walikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wakati walipotumbuiza kwenye onyesho la 'Tamsha la Wajanja' lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Nyota hao waliibua shangwe na nderemo kubwa kutoka kwa mashabiki baada ya kupanda jukwaani na kuimba kwa kupokezana wimbo walioshirikiana uitwao 'Nidanganye'.
Mbali na Diamond na Shetta, wengine walioshangiliwa sana na mashabiki ni pamoja na Fid Q na Ommy Dimpoz aliyechengua kwa nimbo zake za 'Baadaye' na 'Nai Nai'.
Mkuu wa kitengo cha mahusiano na mawasiliano cha kampuni ya huduma za simu ya Vodacom ambao ndio waandaaji wa onyesho hilo, Joyclyine Kamuhanda, alisema kuwa onyesho hilo limelenga kuwaweka pamoja Watanzania na pia kuwawezesha kuwashuhudia wanamuziki hao waliowachagua.
Aliongeza kuwa baada ya onyesho hilo kufanyika Dar Es Salaam na Morogoro, wanatarajia kwenda katika mikoa mingine kama Tanga (Julai Mosi) na Mtwara ambako watafanya onyesho hilo Julai 8.

Sunday, June 24, 2012

Tume ya Warioba kutafuna bilioni 40/-

 Kwa mwaka kila mjumbe kuvuna zaidi ya milioni 300/-
  Wasio wajumbe yaani watumishi kutumia bilioni 4.3/-
  Sh bilioni 2.0 kulipia nyumba wafanyakazi wa Sekretariati

Jaji Joseph Warioba
Serikali imefanya kufuru ya kutenga Sh. bilioni 40/- kwa ajili ya wajumbe 34 wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba. Kwa mujibu wa kasma ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoko kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13.
Iliyopewa jina la Vote Number 8 (Fungu namba 8), wajumbe 34 wa tume hiyo wametengewa posho ya Sh. bilioni 10 watakayolipwa kwa kipindi cha mwaka mmoja jambo ambalo baadhi ya wabunge wamesema hawaridhiki na kuhoji serikali inatafuta kitu gani kwa tume hiyo.
Wajumbe wa kawaida wa tume hiyo kwa mujibu wa mchanganuo wa bajeti, watalipwa posho ya Sh. karibu 450,000 kwa siku lakini Makamu Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Tume fungu lao ni kubwa zaidi ambalo limeongezewa viburudisho na takrima.
Kwa mujibu wa taarifa za uchambuzi wa posho hizo, kila mjumbe kuanzia mwaka wa fedha wa Julai 2012 hadi Julai 2013, atakuwa amejikusanyia zaidi ya Sh milioni 294 jambo ambalo baadhi ya wabunge waliohojiwa na NIPASHE Jumapili walisema ni maajabu ya Firauni.
Pamoja na kuhakikishiwa kuwa na ukwasi mkubwa, pia wametengewa Sh. milioni 10 kwa ajili ya matibabu kwa wale ambao wameelezwa kuwa hawapo kwenye utaratibu wa kugharamiwa tiba na serikali.
Dau kubwa ambalo lipo kwenye bajeti hiyo kwa mujibu wa wabunge hao ambao wameomba majina yao yasitajwe, ni kutengwa Sh. milioni 250 zinazodaiwa zitatumika kwa ajili ya usafi na ulinzi wa ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Wajumbe hao 34 kutoka Bara na Visiwani wametengewa Sh milioni 10 kugharamia mazishi na kuwasafirisha wajumbe wa tume hiyo watakaofariki dunia wakati wakiwa kwenye mchakato wa kukusanya maoni.
Sambamba na hilo, tume hiyo imetengewa zaidi ya Sh. bilioni 10 kununua magari 56 ambayo sita kati yake ni Land cruiser heavy duty zenye mikonga zitakazofungwa vipaza sauti ili kukusanya watu watoe maoni yao na mengine 50 yatakuwa ni mashingingi ya kisasa maarufu kama V8. Kwa sasa tume hiyo inadaiwa kuazimwa magari kutoka Wizara ya Sheria na Katiba.
Baadhi ya wabunge waliliambia gazeti hili kuwa bajeti na idadi ya magari imepunguzwa badala ya kutumia Sh. bilioni 10 zitatumika Shilingi bilioni sita na kwamba yatakayonunuliwa ni magari 26 badala ya 56 lakini idadi ya Land cruiser heavy duty zitakazofungwa vipaza sauti haijabadilika.
Ofisi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pia inatarajiwa kutumia Sh milioni 256 kugharamia umeme na maji ambapo kila huduma imepangiwa kugharimu karibu Sh milioni 128, yaani umeme Sh. 127,992,000 kadhalika maji nayo yamepangiwa kugharimu kiasi hicho na kuwafanya wabunge wachambuzi kuhoji sababu za gharama za umeme na maji kufanana.Tume hiyo imetengewa posho ya takrima iliyoitwa hospitality services ya jumla ya Sh. milioni 300 huku simu za TTCL pamoja na gharama za nukushi (fax) zikifikia karibu Sh. milioni 127 wakati zile za mkononi zitawagharimu walipa kodi zaidi ya Sh. milioni 91.2.
WAFANYAKAZI WA SEKRETARIATI YA TUME
Kundi hili sio la wajumbe bali hawa ni watumishi wa ofisini watawala, wahasibu, makatibu muhtasi, wafagizi, wataalamu wa kompyuta, madereva na wengine nao wametengewa mafungu kadhaa ikiwemo posho ya kujikimu wakisafiri nayo ni Sh bilioni 4.3.
Kingine ambacho wabunge waliochambua Vote No 8 ama fungu hilo walisema kilichowashangaza ni kutenga Sh bilioni 2.0 kwa ajili ya kulipia nyumba za wafanyakazi wa Sekretariati ya Tume na kuhoji hivi wafanyakazi hao hawana nyumba jambo lililoelezewa na wawakilishi hao wa wananchi kuwa ni ulaji ambao wanasubiri kuuhoji wakati serikali ikiwasilisha bajeti hiyo.
Pia wafanyakazi hao ambao watalipwa posho ya Sh. 50,000 kwa siku wametengewa Sh. milioni 300 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chai ambavyo havikuelezwa ni vitu gani pamoja na vitafunwa. Tume ya Mabadiliko ya Katiba inaongozwa na Jaji Joseph Warioba ambaye ni Mwenyekiti wakati Makamu Mwenyekiti ni Jaji Augustine Ramadhani.

Miss Dar Intercollege kujulikana leo

 
Mrembo atakayefanikiwa kuibuka mshindi katika shindano la Miss Dar Intercollge mwaka huu ambalo linafanyika leo Ijumaa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala la Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), atazawadiwa fedha taslimu Sh. 500,000 pamoja na gauni lenye thamani ya Sh. 500,000 kutoka kwa mbunifu maarufu wa mavazi nchini, Mustafa Hassanali.

Mratibu wa shindano hilo, Dina Ismail, alisema jana kwamba maandalizi ya shindano hilo litakalopambwa na mshindi wa tuzo tatu za Kili Music Nassib Abdul ‘Diamond’ yamekamilika ambapo warembo 14 kutoka vyuo mbalimbali watachuana.

Alisema mshindi wa pili atazawadiwa Sh. 350,000 wakati  mshindi wa nne na wa tano kila mmoja atazawadiwa Sh. 200,000, huku washiriki watakaosalia kila mmoja atapata kifuta jasho cha Sh.150,000.

Aliwataja warembo watakaochuana kuwania taji hilo kuwa ni pamoja na Neema Michael(CBE), Jamila Hassan (DSJ), Natasha Deo, (Ustawi), Diana Nyakisinda (DSJ), Saada Seleman, Rose Masanja (Ustawi), Sharifa Ibrahim (DSJ), Nancy Maganga (Ustawi), Rose Mushumbushi (CBE), Veronica Yolla (DSJ), Veronica Ngota (CBE), Jaquline Cliff (DSJ), Catherine Christian (OUT) na Hilda Edward (Ustawi).

Thursday, June 21, 2012

Ajali yaua sita Dar

Watu wapatao sita wanahofiwa kufa katika ajali iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Tegeta Kibaoni baada ya gari aina ya Scania lililokuwa likitokea kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill kupata hitilafu ya breki na kugonga daladala aina ya Isusu Journey kisha kuangukia watu waliokuwemo kwenye Baa ya KMM.

Mtei akoleza moto wa Mnyika

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akizungumza na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika katika viwanja vya bunge jana. Mnyika amerejea kuhudhuria vikao vya bunge baada ya juzi kutimuliwa bungeni na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai

 MWASISI wa Chadema, Edwin Mtei amemtetea Mbunge wa Ubungo, John Myika kuwa alikuwa sahihi kusema kwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kwa kuwa kuna matukio mengi yaliyohitaji uamuzi wake na hakuutoa kwa wakati.

Pia Mtei amelaumu Kanuni za Bunge zilizomwezesha Naibu Spika, Job Ndugai kumtoa nje ya ukumbi wa Bunge mbunge huyo.

  Juzi, Mnyika alitolewa nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya kukukataa kufuta kauli yake kuwa ‘Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu’.
Akitetea kauli hiyo, Mtei alirejea baadhi ya matukio aliyodai yanaonyesha udhaifu huo, ukiwamo uamuzi ya Rais Kikwete juu ya hatua za kuwachukulia walioiba fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mtei alifafanua kwamba,  kitendo cha Rais  Kikwete kuwataka wezi hao warudishe fedha walizoiba badala ya kuwakamata, kinadhihirisha udhaifu mkubwa wa kiongozi huyo.

  “Rais Kikwete ana udhaifu wa kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanahujumu taifa  kwa ufisadi…udhaifu wa Rais ni kama kutowadhibiti wezi wa fedha zetu kama fedha za EPA. Aliwaambia wezi warudishe fedha, badala ya kuwatia ndani wanabaki wanatamba kwa kuiba fedha zetu,” alisisitiza Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu.

 Alisema kibaya zaidi ni kwamba, nchi inayumba kutokana na uongozi mbovu kuanzia ngazi ya urais hadi chini, kwa kuwa tunaongozwa na watu wasiojua na kuisimamia Katiba.

Kauli kuhusu Bajeti
Akitoa maoni yake juu ya Bajeti ya Serikali ya mwaka huu, Mtei alisema Bajeti hiyo haina jipya kwa kuwa haishughulikii matatizo na kero za wananchi.

Alisema Bajeti hiyo ambayo mjadala wake unahitimishwa kesho, haiwezi kukabilina na mfumuko wa bei unaolikabili taifa.

Kuhusu suala la deni la Taifa linalofikia Sh20.2 trilioni, alisema nchi ipo njia panda, hali ambayo ni hatari kwa kuwa ni mzigo kwa taifa na linazidi kuongezeka kila mwaka.Mwanasiasa huyo ambaye ni Mwenyekiti wa kwanza wa Chadema, aliponda vitendo vya Serikali kukopa fedha kila mara kwenye mabenki ya kibiashara nchini, na kuomba kwa wahisani

UEFA yaitoza faini England

 Mashabiki wa England
Chama cha soka cha England, FA, kimetozwa faini ya Euro 5,000 (sawa na pauni 4000), kutokana na utovu wa nidhamu wa mashabiki wake ambao Ijumaa iliyopita walijaribu kuuvamia uwanja baada ya Engldan kuishinda Sweden.
Faini hiyo ni kufuatia mashabiki kujaribu kuingia uwanjani baada ya England kuishinda Sweden 3-2 katika mechi ya kundi D mjini Kiev.
Chama cha FA kimeamua hakitakata rufaa kuhusiana na faini hiyo, na kwa kuwa UEFA haijaitoza FA pesa nyingi, inaashiria kwamba shirikisho hilo la soka ya Ulaya linalichukua tukio hilo kama jambo dogo.
"Tunakubali hatua iliyochukuliwa, na tunalifikiria tukio hili kama jambo ambalo limetatuliwa," taarifa ya FA ilielezea.
Baada ya magoli ya England yaliyotiwa wavuni na Theo Walcott na Danny Welbeck, mashabiki kati ya 20 hadi 30 walivikaribia vizuizi uwanjani, na kutaka kuingia ndani ya uwanja wa Olympic, lakini walifanikiwa kuifikia sehemu ya riadha tu.
Chama cha FA, kikijitetea, kiliweza kutoa ushahidi thabiti wa video mbele ya UEFA na kuonyesha kwamba “uvamizi” huo ulikuwa ni jambo ambalo lilitokea ghafula, na wala mashabiki hao hawakuwa wamepanga kutekeleza kitendo hicho.
Tukio hilo lilichukuliwa kama jambo dogo, na hata afisa wa UEFA katika mechi hiyo hakulitaja katika ripoti yake kuhusiana na mechi.
Chama cha FA pia kimethibitisha kwamba hakuna mashabiki wa England waliokamatwa aidha nchini Poland au Ukraine katika mashindano ya mwaka huu.

Rooney ni nyota ya England

 Wayne Rooney
Wayne Rooney alikaribishwa kama shujaa katika timu ya England usiku wa Jumanne, baada ya kutokuwepo kwa muda kufuatia adhabu ya UEFA, na bao lake moja dhidi ya Ukraine liliiwezesha timu yake kuwa kileleni katika kundi la D.
Vile vile bao hilo linamaanisha England imeweza kuiepuka Uhispania katika robo fainali, na sasa itacheza dhidi ya Italia.
Rooney, akiwa karibu sana na kipa wa Ukraine, Andriy Pyatov, aliweza kufunga kwa kichwa, mpira uliokuja juujuu kutoka kwa nahodha Steven Gerrard.
Licha ya England kuibuka washindi, Ukraine walifanya juhudi kubwa na kupata nafasi nyingi zaidi za kusawazisha, lakini yote hayo hayakufua dafu.
Ukraine walistahili kupata bao wakati mkwaju wa Marko Devic ilikuwa wazi umevuka mstari, lakini kufuatia juhudi za John Terry katika kuondosha mpira huo, pengine mwamuzi alishawishika kwamba kweli mpira haukuvuka msitari.

Sweden yaondoka kwa kishindo

 Ufaransa na Sweden
Bao lililoingia wavuni kwa ustadi kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic limeisaidia Sweden kuishinda Ufaransa magoli 2-0 katika mechi ya kundi D usiku wa Jumanne, na kuhakikisha wameisukuma Ufaransa katika nafasi ya pili katika kundi, na pia kuilazimisha kukutana na mabingwa watetezi Uhispania katika mechi ya robo fainali ya Euro 2012.
Ufaransa walilemewa katika mechi hiyo, na Ola Toivonen alikaribia kuiletea Sweden bao la kwanza alipogonga sehemu ya nje ya mwamba wa goli.
Hatimaye Ibrahimovic alipata bao kupitia mkwaju kutoka yadi 15, baada ya kusukumiwa mpira kutoka kwa Sebastian Larsson.
Olivier Giroud alifunga kwa kichwa na kuiwezesha Sweden kupata bao lao la pi
Kushindwa kwa Ufaransa kuna maanisha hatua yao ya kucheza pasipo kushindwa katika msururu wa mechi 23 zilizopita tangu waliposhindwa wakiwa nyumbani na Belarus mwezi Septemba mwaka 2010 imesitishwa.
Huo ndio muda mrefu zaidi ulioandikishwa timu kucheza pasipo kushindwa kwa upande wa mechi za kimataifa.
Ufaransa wameshindwa baada ya mechi 24 za kimataifa, na kocha Laurent Blant sio tu atakuwa na wasiwasi katika kupambana na mabingwa wa Ulaya na wa dunia pia, bali pia kuhusiana na timu yake kucheza mchezo wa kiwango duni.
Sweden tayari walikuwa wameondolewa katika mashindano baada ya kushindwa katika mechi zao mbili za mwanzo, lakini nia yao ilikuwa ni kucheza kadri ya uwezo wao kabla ya kurudi nyumbani.
Jumapili iliyopita, wachezaji hao walikataa ushauri wa meneja Erik Hamren wa kupumzika, na badala yake waliamua kuitumia siku hiyo katika kufanya mazoezi zaidi.

TIMU YA ITALIA ROBO FAINALI

 Italia na Jamhuri ya Ireland
Italia ilipata ushindi dhidi ya timu ya Jamhuri ya Ireland ambayo tayari wachezaji wake walikuwa wanajitayarisha kuondoka kutoka mashindano ya Euro 2012, kwa kuwafunga magoli 2-0.
Jamhuri ya Ireland walianza mchezo huo wa Jumatatu usiku, wakithibitisha nia yao ya kujitahidi kupata ushindi, lakin ni Antonio Cassano, mchezaji wa Italia, ndiye aliyefanikiwa kuliona lango kwanza, akitumia kichwa, kufuatia mpira wa kona iliyopigwa na Andrea Pirlo.
Iwapo Ireland ingelisawazisha, kama alivyokaribia kufunga Keith Andrews lakini kipa wa Italia Gianluigi Buffon akaweza kuokoa, ingelimaanisha Italia, katika kundi C, wangelijikuta wametupwa nje ya mashindano hayo ya Ulaya, hasa kama Croatia ingelipata bao la kusawazisha dhidi ya Uhispania, mechi iliyochezwa sambamba na hii, na iliyokwisha kwa ushindi wa Italia wa bao 1-0.
Andrews aliamrishwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na Mario Balotelli akafanikiwa kufunga bao la pili na kuwatuliza mashabiki wa Italia.
Kutokana na Uhispania kuishinda Croatia, sasa itakutana na mshindi wa kundi D.England ni miongoni mwa mataifa katika kundi hilo.

Pinda aunda Kamati kuokoa Bajeti Kuu

 WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameunda Kamati Maalum ya mawaziri sita kusaidia mchakato wa marekebisho ya Bajeti ya Serikali ambayo mjadala wake utahitimishwa kesho.Kuundwa kwa kamati hiyo kunazifanya kamati zinazoifanyia kazi Bajeti ya 2012/2013 kufikia tatu.

Ijumaa iliyopita wabunge wa CCM waliunda kamati ndogo kwa ajili ya kusaidi pamoja na mambo mengine kuangalia vyanzo vingine vya mapato na kuona iwapo bajeti ya maendeleo inaweza kuongezwa, kukidhi kiu ya wabunge.

Kamati nyingine ni ile ya Fedha na Uchumi ya Bunge ambayo tayari imetoa maoni yake bungeni kuhusu Bajeti, lakini ikabainisha kuwapo kwa kasoro kadhaa ambazo zinapaswa kurekebishwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alikiri kuundwa kwa kamati hiyo, lakini akakataa kutoa taarifa za kina kuhusu suala hilo kwa maelezo kwamba huo ni utendaji wa kawaida wa shughuli za Serikali.

“Sidhani kama hiyo ni habari kubwa ya kwenda kwenye public (kwa umma). Kwanza siyo kamati ya mawaziri, haiwezi kuwa hivyo, na huo ni utendaji wa kawaida wa ndani ya Serikali maana sisi tuna mambo mengi tunafanya,”alisema Lukuvi na kuongeza:

“Kamati za utekelezaji wa shughuli za Serikali ziko nyingi sana na siyo tu za Bajeti. Kwa hiyo ndio maana nakwambia hilo ni jambo dogo sana ambalo mimi sidhani kama linahitaji kutangazwa, kama lingekuwa hivyo mimi ningekuwa wa kwanza kutaka kulizungumzia,” alisema.

Kazi ya Kamati

Habari ambazo Mwananchi limezipata zinasema kwamba kamati ya mawaziri nayo inafanya kazi ya kubuni vyanzo vingine vya mapato ya Serikali, ili kufidia pengo la baadhi ya kodi ambazo zinatarajiwa kufutwa kutokana na shinikizo la wabunge.

Miongoni wa kodi hizo ambazo huenda zikafutwa wakati Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa atakapohitimisha Bajeti yake kesho, ni ile inayopendekezwa kuongezwa kwenye muda wa maongezi ya simu na ile ya inayopendekezwa kutozwa kwa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda.

Kadhalika, kamati hiyo ya mawaziri imepewa jukumu la kuona iwapo itaweza kushauri uwezekano wa kuongezwa Bajeti ya sasa ya maendeleo kutoka asilimia 30 inayopendekezwa na Serikali, jambo ambalo pia limekuwa likipigiwa kelele na wabunge wengi.“Hatuwezi kufumua Bajeti nzima ila kusema kweli ni kwamba lazima kutakuwa na mabadiliko mengi, tatizo kubwa ambalo linatuumiza vichwa, tunajiuliza kama tunaweza kupata hiyo nyongeza ya hizo fedha za maendeleo walau Sh500 bilioni,”alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

Taarifa zaidi zimewataja wajumbe wanaounda kamati hiyo ambayo ilifanya kikao chake cha kwanza juzi kuwa ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk Mgimwa, Lukuvi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Wengine katika kamati hiyo iliyoundwa kwenye kikao cha kazi cha Baraza la Mawaziri, Jumamosi iliyopita chini ya Pinda, ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, Naibu Waziri wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Adam Malima na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Habari zaidi zilidai kuwa mawaziri hao watafanya kazi hiyo sasa na hata baada ya Bunge la Bajeti ili ushauri wao uweze kuzingatiwa katika maandalizi ya bajeti ijayo ya 2013/2014.

“Tunawatarajia kwamba watatusaidia hata katika bajeti za kisekta zinazokuja,” alisema mjumbe mwingine wa kikao hicho.

Wasiwasi ulikuwa ni iwapo ushauri wa kamati hiyo utaweza kuzingatiwa katika majumuisho ya Waziri wa Fedha na Uchumi wakati atakapohitimisha Bajeti yake, lakini jana Spika wa Bunge, Anne Makinda alifungua milango inayowezesha Serikali kuongeza vyanzo vipya vya mapato hata baada ya Bajeti Kuu kupitishwa.

Uamuzi wa Bunge

Jana Spika Makinda alisema Bunge limeahirisha kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria za Fedha wa mwaka huu, na sasa muswada huo utapitishwa mwishoni kabisa mwa Mkutano wa nane Bunge.

Hatua hiyo ni dalili kwamba Serikali sasa iko tayari kufanya marekebisho makubwa ya Bajeti yake na hata zile za kisekta, hasa katika maeneo ya kuongeza vyanzo vipya vya mapato kadri Kamati za Bunge, wabunge na Kambi ya Upinzani watakavyopendekeza.

Kusogezwa huko pia kumewezesha kuongezwa siku moja ya majadiliano ya hotuba ya Bajeti kutoka siku nne hadi tano, pia unatoa fursa ya Serikali kuongeza vyanzo vyake vya mapato kwa kuzingatia maoni, mawazo na ushauri wa wabunge.

Muswada wa Sheria ya Fedha ulikuwa umepangwa kuwasilishwa kesho kama hitimisho la mjadala wa Bajeti ya Serikali, lakini sasa umepelekwa mbele kutokana na kile Makinda alichosema kuwa ni kutoa fursa kwa wabunge kuishauri Serikali kuhusu vyanzo vipya vya mapato.

Makinda alisema uamuzi huo ulifanywa katika kikao cha Kamati ya Uongozi cha Juni 18, mwaka huu baada ya kuzingatia maoni ya wabunge, Serikali na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ambao walitaka kuahirishwa kwake, ili kuruhusu Serikali kuongeza vyanzo vya mapato kadri itakavyoshauriwa na wabunge.
 Aliongeza kuwa Bunge limeridhika kwamba licha ya kutopitishwa kwa muswada huo mapema kama inavyotakiwa, bado Serikali itaweza kukusanya kodi kwa kutumia sheria nyingine za nchi zilizopo.

Mabadiliko hayo ni mwanzo wa mchakato wa mabadiliko ya Kanuni za Bunge ili kuwezesha vikao vya Bunge la Bajeti kufanyika mapema na kuhitimishwa Juni 30, ili kuruhusu Serikali kuanza mwaka wa fedha baada ya Bajeti nzima na Sheria ya Fedha kuwa vimepitishwa.

“Mabunge mengi ya Jumuiya ya Madola yana utaratibu wa kupitisha Muswada wa Sheria ya Fedha na Muswada wa Mutumizi mwishoni kabisa mwa mjadala wa Bajeti. Lakini tumefuatilia na kubaini kuwa mchakato wa kupitia Bajeti ya Serikali huanza mapema na kumalizika kabla ya mwaka mpya wa fedha kuanza,”alisema Makinda na kuongeza:

“Bunge letu lingepaswa liwe linakutana na kuanza mchakato wa kupitia Bajeti ya Serikali mapema, ili inapofika Juni 30, mkutano wa Bajeti uwe umemalizika na Muswada wa Sheria ya Fedha kuanza kutumika ifikapo Julai Mosi ambapo mwaka mpya wa fedha unaanza”.

Alisema kutokana na hali hiyo Kanuni za Bunge zitaendelea kufanyiwa marekebisho ili mikutano ya Bunge la Bajeti iweze kuanza mapema kama ilivyo katika nchi nyingine za Jumuiya ya Madola.

Kwa upande Lukuvi, alisema uamuzi wa Serikali kukubali hoja ya kusogezwa mbele muswada huo, ni kutoa fursa ya kuzingatiwa kwa maoni ya wabunge na kuendelea kuibuliwa kwa vyanzo vipya vya mapato.

“Kama Serikali isingekubali, basi ujue hilo la kuahirisha muswada lisingewezekana kabisa, maana ukishapitisha Muswada wa Sheria ya Fedha hata maoni yatakayoendelea kutolewa kwenye bajeti nyingine yangekuwa hayana maana,” alisema Lukuvi.

Mbunge alipua mawaziri

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), amewataka wabunge kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kuikataa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2012/13, kwa kuwa mawaziri wake wameshindwa kumsaidia kuleta Bajeti ambayo inajibu matatizo ya Watanzania.

Alitoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mjadala wa Bajeti na baadaye kutoa ufafanuzi wa kauli yake nje ya Bunge, kuwa mawaziri wa Kikwete wameshindwa kumsaidia, kwani wametenga fedha nyingi katika matumizi mengineyo na kutelekeza mpango wa Serikali wa Miaka Mitano.
 

Saturday, June 16, 2012

Miss Tanzania kupatikana leo

MREMBO bora wa Tanzania atakayekwenda kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya urembo dunia, anatarajia kujulikana leo katika shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa 327, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Shindnao hilo la dunia linatarajia kufanyika Agosti 18 nchini China.
Warembo 10 wanatarajia kujipanga ukumbini kuwania kushinda taji hilo na baadaye kuwaikilisha nchi kwenye mashindano ya urembo ya dunia.
Mratibu wa Shindano hilo, Hashim Lundenga aliiambia Mwananchi maandalizi kuwa, maandalizi yote yamekamilika na mshindi atajinyakulia Sh2 milioni.
"Unajua shidano la dunia hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba, lakini kwa sasa linafanyika mapema zaidi kutokana na mabadiliko ya kalenda," alisema Lundenga.
Walimbwende watakaopanda jukwaani leo ni pamoja na Pendo Laiser, Lisa Jensen, Christine Willium, Jenifer Kakolaki, Gloryblanca Mayowa, Hamis Hasan, Queen Saleh, Mwajabu Juma, Neema Saleh na Stela Mbuge.

Diamond kutumbuiza Miss Arusha

 
Aidha aliwataja watumbuizaji kuwa ni pamoja na msanii Diamond atakayebeba onyesho zima kwa upande wa burudani ambaye atasindikizwa na kikundi cha ngoma na kudansi cha Boda2Boda cha mkoani hapa pamoja na msichana Sister P wa mkoa wa Arusha ambaye ni mwimbaji wa miondoko ya reggae.

Alisema kuwa jumla ya warembo 20 kutoka vitongoji vinne vya mkoa wa Arusha wameingiaa kambini kujiandaa na shindano hilo. Alisema warembo hao ni washindi wa kutoka vitongoji vya Miss Arusha City Centre, Njiro, Sakina na Monduli.

"Kwa kweli sio kama najisifu ila warembo wetu ni wazuri na nina imani watashinda maana wana upeo, elimu ya kutosha na maadalizi ni mazuri.

"Kingine kikubwa mwaka huu ni kwamba mashindano haya yatakuwa tofauti sana kwani tumejipanga vilivyo na hatutaki kufanya makosa.

Kwanini kila siku taji liende Dar na Mwanza tu, safari hii nitahakikisha linakuja Arusha," alisema Mwandago.

Aliwataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni TBL, Dodoma Wine, Tanzanite One, Mogaben Priters, Libeneke la Kaskazini blog na Arusha Traveling Lodge ambao ndio wametoa kambi ya warembo.

Wabunge CCM wapinga Bajeti

 KAMATI ya wabunge wa CCM jana ilikutana kwa zaidi ya saa tano katika kikao ambacho wabunge hao waliibua hoja ya kutaka kuchunguzwa kwa Mfuko Mkuu wa Serikali kwa maelezo kwamba kuna dalili za kuwapo kwa ufisadi.Habari kutoka ndani ya mkutano huo ulioongozwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zilisema msingi wa hoja hiyo iliyotolewa na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ni kutokuwapo kwa uwiano kati ya fedha zilizokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) pia kutoka kwa wahisani, na zile zilizopelekwa katika wizara na Idara za Serikali.

Katika hoja hiyo ambayo iliripotiwa kwamba iliungwa mkono na wabunge wengine kadhaa, Ole Sendeka alipendekeza iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mfuko huo au iteuliwe Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Hesabu kufanya ukaguzi.

“Tumeshindwa kuelewa inakuwaje TRA inakusanya mapato asilimia 106, yaani zaidi ya asilimia 100, wahisani tunaambiwa wametoa fedha asilimia 80,halafu eti fedha za maendeleo zilizopelekekwa wizarani ni asilimia 22 tu, haiwezekani na hapa tunataka uchunguzi ufanyike,”alisema mmoja wa wabunge wa CCM.

Mbunge mwingijne alisema wamebaini kwamba taarifa ya Waziri wa Fedha kuhusu fedha zilizotolewa kwa mujibu wa bajeti ya 2011/2012 zinatofautina na uhalisia katika wizara ya idara za Serikali na kwamba hiyo ni dalili kwamba hizo ni dalili ya kuwapo kwa matundu kwenye hazina hiyo ya nchi yanayopaswa kuzibwa.

“Tumesema haiwezekani, tunahitaji kutekeleza Ilaani ya CCM na ahadi ambazo sisi wabunge, Rais na chama tulizitoa kwa wananchi, sasa kama tunapitisha bajeti, fedha zinakusanywa, lakini hazifiki kwa wananchi ndiyo tunafanya kazi gani? Hili tunasema haliwezekani,”alisema mbunge mwingine baada ya kikao hicho jana jioni.

Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho kilichoanza saa 5.30 asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa na kumalizika saa 11.30 jioni ziliwataja baadhi ya wabunge waliounga hoja mkono hoja hiyo kuwa ni Alphaxard Lugora (Mwibara), Godfrey Zambi (Mbozi Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera).

Bajeti 2012/2013
Kuhusu Bajeti ya 2012/2013, wabunge hao wa chama tawala wanaelezwa kwamba waliigeukia Serikali wakieleza kutoridhishwa na bajeti iliyowasilishwa bungeni juzi jioni na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa.

Miongoni mwa malalamiko makubwa ya wabunge ni hao ni kutozingatiwa kwa vipaumbele vya Taifa pia Mpango wa  wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011 - 2016 ambao ulipitishwa na Bunge mwaka jana.kwenye bajeti, tunayaona mambo mengi kuwa ni danganya toto tu, tumejadili, lakini sijui kama kipo cha kubadilika,”alisema mmoja wa wabunge waliohudhuria kikao hicho.

Habari zaidi zilidokeza kuwa Waziri Mkuu Pinda alilazimika kutoa nafasi kwa kila mbunge aliyeomba nafasi ya kuzungumza ili kupunguza hasira ambazo zingeweza kujitokeza kwenye mjadala wa jumla keshokutwa.

“Ndiyo maana tumechukua masaa, Pinda ameamua kuwapa watu wote nafasi ili wazungumze, ila mimi nimetoka wala sikuchangia kitu nasubiri huko ndani Jumatatu au Jumanne nikipata nafasi,”alisema Mbunge mwingine.

Mbunge wa Viti Maalum, Sara Msafiri aliripotiwa akipinga ushuru kwenye muda wa maongezi ya simu na kutaka Serikali kuhakiki kwanza mapato ya kampuni za simu.

Kadhalika mbunge huyo alinukuliwa ndani ya kikao hicho akisema bajeti hiyo imejaa maslahi ya wakubwa tu, na kwamba lazima yafanywe marekebisho ambayo yataifanya ishuke chini kwa wananchi.
Mwingine ni Naibu Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba ambaye alinukuliwa akiishauri Serikali iwe wazi kuhusu msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifaa vya gesi kwani mwanya huo unaweza kutumiwa vibaya kukwepa kodi.

Kadhalika Makamba alinukuliwa akitaka kubadilishwa kwa taratibu za kutoza kodi kampuni za mafuta kwa kuweka utaratibu wa kodi kulipwa baada ya biadhaa hiyo kuingizwa nchini badala ya siku 45 za sasa.

“Kwanini tuwape hawa wafanyabiashara mitaji kwasababu utaratibu wa sasa wanaingiza mafuta hata kama hawana senti tano, na sisi tunakubali kuahirisha kuchukua kodi hadi baada ya siku 15 na baadaye siku 30. Hili ni tatizo na tuangalie eneo hili vizuri,”chanzo chetu kilimnukuu Makamba akisema katika kikao hicho.

Kutokana na hoja za wabunge hao, Kikao hicho kiliazimia kuundwa kwa kamati ndogo ya wabunge wa CCM kuangalia jinsi ya kupanua wingo wa kukusanya mapato pia kupendekeza mgawanyo wa mapato hayo tofauti na Bajeti ya Serikali.

Baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi aliwaongoza wajumbe wa kamati yake kwenda kukutana tena na Waziri wa Fedha ili kuangaliwa kama wanaweza kufanya marekebisho ya bajeti hiyo kwa kuzingatia maoni ya wabunge wa CCM.

Mpina apinga hadharani
Wakati hayo yakiripotiwa kutokea ndani ya kikao cha wabunge wa CCM, Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina jana alijitokeza mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma na kusema kwamba hataunga mkono bajeti hiyo na kwa maana hiyo “yupo tayari kufukuzwa” kutokana na uamuzi wake huo.

Licha ya kutangaza kutoiunga mkono bajeti hiyo, mbunge huyo alisema keshokutwa Jumatatu ataomba mwongozo kwa Spika kutoa hoja ya kuomba bajeti hiyo irejeshwe serikalini  ili ifanyiwe  marekebisho na kama Serikali ikiing’ang’ania ni bora Rais Jakaya Kikwete avunje Bunge na kurejewa uchaguzi.
Hata hivyo, alisema anaamini kwamba hatua ya kuvunja Bunge haiwezi kufikiwa ikiwa busara itatumika kumaliza mvutano uliopo.

Mpina alisema Bajeti ya Serikali inakiuka azimio la Bunge la kutengwa fedha walau asilimia 35 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi alisema yapo makubaliano ya wabunge kwamba kila mwaka wa fedha, zitatengwa Sh2.7 trilioni kutoka fedha za ndani kugharamia miradi ya maendeleo ili kuwezesha fedha hizo kufikia walau asilimia 35 ya bajeti.

Alisema kwa mshangao bajeti iliyowasilishwa juzi iliweka kando mapendekezo na maazimio ya wabunge.
“Bajeti hii, tuliikataa katika kamati yetu, kwa kuwa inakiuka Azimio la Bunge na pia mpango wa serikali wa miaka mitano, na juzi iliposomwa niliomba Mwongozo wa Spika ili niitake Serikali irudishe bajeti hii na kurekebisha,  lakini bila kufuata kanuni spika alinizuia kwa madai kuwa siku ya kusomwa bajeti hakuna mwongozo” alisema Mpina.

Mpina alisema, kanuni ya bunge ya 68 kifungu cha 7, inaeleza wazi kuwa mbunge, anaweza  kusimamia wakati wowote anapoona hakuna mtu anayeongea.

“Naamini Spika hakunitendea haki na Jumatatu pia nitaomba mwongozo tusiendelee na mjadala wa bajeti hii na kama itaonekana  kutetea fedha kupelekwa kwenye maendeleo ni  kosa hasa wakati ni utekelezaji wa ilani ya CCM, nipo tayari kwa lolote,”alisisitiza.

Alisema kitendo cha Serikali kutenga Sh 2.2 trilioni badala ya Sh2.7 trilioni  ambao ni upungufu wa Sh500 bilioni, kumesababisha miradi mingi kutengewa fedha kidogo na mingine kukosa fedha kabisa.
Alisema  kibaya zaidi mapato ya ndani yameongezeka kwa kiasi cha Sh1.5 trilioni, lakini fedha hizo zimeliwa na matumizi ya kawaida ambayo yameongezeka kwa Sh1.9 trilioni, huku fedha za maendeleo zikipungua kwa Sh397.8 bilioni ikilinganishwa na mwaka 2011/12.

Mpina alisema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikiahidi kupunguza matumizi ya kawaida ili kuongeza kasi ya utoaji huduma na uwekezaji katika sekta zinazokuza uchumi na kupunguza umasikini, lakini hakuna kinachotekelezwa.

 “Matumizi kama haya ya safari, posho,mafuta,ununuzi wa magari , samani, mawasiliano, sherehe,warsha ,makongamano,mafunzo,nje ya nchi yanaweza kuepukika,kupounguza au kuahirishwa”alisema  Mpina.

 Mbunge huyo alihoji inakuwaje  serikali ilipata fedha za  kufidia   mabenki na wafanyabiashara walioathirika na mtikisiko wa uchumi Sh1.7 trilioni halafu  ishindwe kupata Sh500 bilioni kugharamia miradi iliyoainishwa katika mpango wa maendeleo.
“Wewe bwana wewe, sijui nikwambie nini, lakini wabunge tumesema tumechoka, maana hakuna mabadiliko

Sunday, June 10, 2012

kumbe John Travolta ni shoga.....!

 
LOS ANGELES, MAREKANI
BAADA ya wanaume watatu kufichua habari kuwa mwigizaji, John Travolta ni shoga, mtu mwingine wa karibu ameibuka na kuthibitisha habari hizo akisema ni za kweli.

Rubani binafsi wa Travolta, Doug Gotterba, amesema alikuwa na uhusiano na mwigizaji huyo kwa miaka sita kabla hajamuoa, Kelly Preston mwaka 1991.

Doug anasema kuwa uhusiano wake na Travolta ulivunjika baada ya kuoa, kwani makubaliano yao yalikuwa kila mmoja asiwe na mwanamke.

Mpaka sasa Travolta hajajitokeza kuzungumzia kashfa hizi ingawa timu ya wanasheria wake imekanusha tuhuma hizo na kusema zinasukwa na watu wanaotaka kumharibia mteja wao.

Saitoti afariki kwenye ajali ya ndege

 Prof George Saitoti
Prof George Saitoti
Habari kutoka Kenya zinasema kuwa Waziri wa Usalama wa Ndani ,Profesa George Saitoti, na naibu wake, Orwa Ojode, wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi katika eneo la Kibiku karibu na mji wa Ngong, takriban kilometa ishirini kutoka mji wa Ngong.
Abiria wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo wanaarifiwa kuteketezwa kwa kiasi wasichoweza kutambulika.
Kamishna wa polisi Mathew Iteere anaarifiwa kulekea katika eneo la ajali hiyo.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema ndege ilishika moto ilipogusa ardhi kwenye eneo la Ngong Hills.
Bwana Saitoti aliwahi kuwa makamo wa rais na waziri wa fedha katika serikali ya Rais Moi, na akitarajiwa kugombea urais katika uchaguzi ujao.


Mawaziri waijibu Chadema

 Waeleza walivyojipanga kutatua kero
  
Mbowe ajibu hoja zilizoibuliwa na CCM

Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, wakionyesha bango lenye ujumbe wa amani na maendeleo yanayotokana na chama hicho cha CCM, kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam jana.
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimetumia mtaji wa mawaziri wake watano kujibu mapigo ya Chama cha Chadema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa kuzitolea ufafanuzi kero mbalimbali zinazilikabili Jiji la Dar es Salaam na taifa na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Ikiwa ni wiki mbili baada ya Chadema kutoka mashambulizi kwa serikali, mawaziri hao wamejitokeza kujibu mapigo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na CCM kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, eneo ambalo Chadema walilitumia kurusha mashambulizi hayo na kuzindua mpango wao ujulikanao kama Movement for change (M4C).
Akizungumza kwenye mkutano huo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema moja ya kero inayolikabili jiji la Dar es Salaam ni jeuri ya baadhi ya wamiliki na wafanyakazi wa daladala ambao hupandisha nauli bila kufuata utaratibu uliowekwa na serikali.
Dk. Mwakyembe alisema wiki mbili zilizopita, taasisi iliyo chini ya wizara yake, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) walikamata daladala 19 kwa kuongeza nauli kinyume cha sheria.
“Katika kujiridhisha nikasema siwezi kwenda Bungeni nikaacha hali ya Dar es Salaam ni mbaya kwa upande wa nauli, nikapanda daladala kutoka Mwenge kwenda Tegeta na Tegeta kwenda Bunju, badala ya nauli ya Sh. 500 kutoka Mwenge kwenda Tegeta nikatozwa Sh. 1000, kutoka Tegeta mpaka Bunju nilitozwa sh. 1,500, huku ni kuwaumiza wananchi na kuchezea sheria za nchi,” alisema Dk. Mwakyembe.
Alisema watu wanapandisha nauli utadhani wizara yake haipo, na kuahidi kuwashukia wamiliki wa daladala na kwamba watakosa mahali pa kukimbilia na atalazimika kuchelewa kwenda bungeni ili kuhakikisha kero hii inapatiwa ufumbuzi haraka.
Waziri Mwakyembe alisema hakuna sababu ya watu kupandisha nauli ovyo ovyo kama vile serikali imekwenda likizo wakati upo utaratibu wa kisheria wa kufanya hivyo.
“Na sio huko tu kwenye daladala na wengine wote wanaopandisha nauli ovyo kwa kisingizio cha gharama zimepanda, kuna utaratibu wa kisheria kupandisha gharama, kama una maombi yako peleka Sumatra, Sumatra wataitisha mkutano wa wadau, watajadiliana itarudi kwetu, tutaliangalia kama kweli gharama zimepanda halafu tutatoa bei elekezi, sio kila mtu kujiamulia tu, hii ni serikali,” alisema Dk. Mwakyemba.
Dk. Mwakyembe ambaye alikuwa kivutio kwenye mkutano huo kutokana na msimamo wake, alitumia fursa hiyo kutoa namba yake ya simu ya mkononi ya 0782 242526 akiwataka wananchi wampigie wakati wowote wanapoona daladala inawadhulumu kwa kuwatoza nauli kubwa ambayo haipo kisheria.
Akizungumzia tatizo la msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam, alisema foleni zilizopo kimsingi zinaua uchumi wa nchi hasa ikizingatiwa kwamba mkoa wa Dar es Salaam ndio tegemeo la kiuchumi nchini.
Alisema katika kukabiliana na kero hiyo, wizara yake imejipanga katika mwezi mmoja ujao kuanzisha usafiri wa treni wa Tazara kutoka Mwakanga hadi Kurasini kila asubuhi na kutoka Ubungo Maziwa hadi Stesheni, ambapo wataalamu wake wamemuambia huduma hizo zitabeba zaidi ya abiria 9,600 kwa mkupuo.
Aidha alisema wakati anaingia wizarani alikuta wawekezaji wanaotaka kuendesha huduma ya treni, lakini amewapiga ‘stop’ na kwamba kazi hiyo itafanywa na Watanzania wenyewe kupitia serikali yao.
Kuhusu Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), alisema haja ridhika kabisa na utendaji kazi wa mamlaka hiyo na amewapa muda wajiandae kabla hajafanya ziara rasmi kwani anazo taarifa kuwa wafanyakazi wake wamegeuka wafanyakazi wa ‘super market’ ya kuuza 'spare parts' ya magari kutoka nje.
Dk.Mwakyembe alisema watendaji wote wanaofanya biashara hiyo atawashughulikia kwa kuwang’oa hata kama wanajiona ni wakubwa kuliko mti wa Mbuyu.
“Nawakumbusha wenzangu wa bandari ya Dar es Salaam ambayo inatakiwa kuwa sifa na kioo cha Tanzania, mimi sijaridhika nayo kabisa na nimefanya makusudi sijaenda kuwatembelea pale, nataka wajipange sawasawa wasije wakanilaumu mbele ya safari,” alisema huku akishangiliwa na umati wa mashabiki na wanachama wa CCM.
Alisema Tanzania haiwezi kuwa nchi iliyopewa fursa na Mungu kuweza kuwa na lango kuu la nchi sita zinazohitaji huduma hapa lakini nchi hizo zinaikimbia Tanzania kwa sababu ya upuuzi unaofanywa na baadhi ya watendaji wa bandari hiyo.
Dk.Mwakyembe aliwaomba wananchi katika kipindi atakachokuwa katika wizara hiyo hatua atakazokuwa anazichukua dhidi ya watendaji wasiowaaminifu wasiwe wanalalamika na kwamba atatumia miezi mitatu kusafisha uozo uliopo katika wizara na taasisi zake.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wasira, alianza kwa kuwashangaa watu wanaosema kuwa serikali ya CCM haijafanya kitu kwa Watanzania tangu wakati wa uhuru.
Alisema suala la kupanda kwa bei za vitu kama mafuta, si la CCM kwani linaanzia nchi za Uarabuni ambako mafuta hutoka huko na kulifanya tatizo hilo la kidunia zaidi.
“Wapo watu wanasema hili tatizo la ugumu wa maisha ndiyo sera ya CCM lakini tujiulize kwani mafuta yakipanda bei Uarabuni, je! CCM iko Uarabuni? Alihoji Wasira na kuongeza kuwa serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na hali hiyo.
Alisema wanaolalamikia suala la ugumu wa maisha ni kwasababu tu hawajui kwani Tanzania huwezi ukalinganisha na nchi ambazo zipo katika kundi la G8 ambazo uchumi wake upo juu.
Wasira alisema hata hivyo zipo hatua kadhaa zinazochukuliwa na serikali ambapo miongoni mwa hatua hizo ni kuwekeza kwenye kilimo cha mabonde ya Kilombero ambako hekta 100,000 zimetengwa kwa ajili ya kilimo cha mpunga.
Kuhusu kukabiliana na tatizo la kupanda kwa bei ya sukari nchini, alisema katika bajeti ya mwaka huu serikalini imeainisha mabonde ya Kilombero, Rufiji, Wami, Maragarasi na Kagera kwa ajili ya kujenga viwanda vya kuzalisha sukari.
Tatizo la kupanda kwa gharama za umeme, Waziri huyo alisema kuanzia mwezi Julai mwaka huu kutajengwa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dare s Salaam ambapo gesi hiyo itatumika kwa ajili ya kuzalisha umeme na hivyo kupunguza gharama ya nishati hiyo kutoka dola senti 42 hadi kufikia dola senti saba za Marekani.
Alisema watu wanaosema kuwa serikali ya CCM haiwajali wananchi wake na haina lolote inachowafanyia, ni sawa na kufuru.
“Nataka kumpa ujumbe Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema) anapo sema hatujafanya lolote anamkufuru baba yake mzazi aliyedai uhuru na Mwalimu Nyerere, namsihi asije akapata laana kwa kauli zake hizo,” alisema Waziri.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, alikiri kuwepo kwa kero nyingi kwenye sekta ya ardhi na kwamba ufumbuzi wa kero hizo umekuwa ukifanywa kwa kuzingatia sheria za nchi zilizopo.
“Katika sekta ya ardhi tunakwenda kwa sheria, na wahahkikishia wananchi hakuna mtu yoyote atakayeporwa ardhi yake bila kulipwa haki yake,” alisema
Profesa Tibaijuka alisema wananchi ambao waliporwa ardhi zao kwa ubabe aidha na watendaji wa kata au vijiji, wapeleke kero hizo ofisini kwake ili aweze kuzifanyia kazi haraka iwezekanavyo.
Naye Wziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, alisema wizara yake imejipanga kutatua kero za maji katika jiji la dare s Salaam na maeneo mengine kama Ilani ya CCM inavyoelekeza ifikapo mwaka 2015 upatikanaji wa maji mijini ifikie asilimia 90 kutoka asilimia 65 za sasa na vijijini kutoka asilimia 50 hadi asilimia 65.
Kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, alisema kuwa wanaupanua kutoka chujio moja hadi matano ambapo gharama zake zitakuwa ni dola milioni 37 na ujenzi huo unatarajiwa kukamilika Machi mwakani hali kadjhalika na ule wa Ruvu Juu.
Alisema katika mwaka wa fedha 2012/13 serikali imetenga sh. bilioni 16 kujenga bomba kubwa lenye upana wa mita 1.8 umbali wa kilomita 58 kutoka Ruvu Chini hadi matenki ya yaliyopo Chuo Kikuu cha dare s Salaam.
Profesa Maghembe alisema katika mwaka huu wa fedha serikali imetenga sh. bilioni 15 kujenga visima eneo la Kimbiji na Nampera hali kadhalika inatarajia kujenga bwawa kubwa la Kidunga mkoani Morogoro lengo likiwa ni kuongeza upatikanaji wa maji katika jiji la dare s Salaam.
Naye Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema kuwa nchi nzima kuna miradi ya barabara yenye urefu wa kilomita 11,154 inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami na kwamba otakapo kamilika hata Chadema wataendeleza maandamano yao kupitia barabara za lami.
Alisema miradi yote hiyo inagharimu kiasi cha shilingi trilioni sita ambapo nusu yake zimetolewa na serikali ya Tanzania.
“Nawapongeza wapinzani, waendelee kuandamana katika barabara za lami maana natambua kuwa shukurani ya punda ni mateke, na wasione vyaelea vimeundwa, pia unaweza kumbeba mtu mgongoni kumvusha mtoni na unapofika ng’ambo na kumshusha anakuambia kwanza mgongo wake ulikuwa unanuka,” alisema.
MBOWE AJIBU MAPIGO
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimejibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Chadema, Freeman Mbowe na Dk Wilbrod Slaa, walitoa majawabu hayo wakati wakihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa Operesheni Okoa Kusini uliofanyika jana kwenye uwanja wa Likangara mjini Ruangwa, mkoa wa Lindi.
Dk Slaa alisema kilichofanywa na mawaziri wa serikali ya CCM ni kutoa maneno yasiyolingana na uhalisia wa mambo yalivyo ndani ya jamii.
“Viongozi waliopo serikalini hawana wajibu wa kupiga maneno, wanatoa kauli zisizolingana na uhalisia wa hali ilivyo, wanachotakiwa kukifanya ni kufanya kwa vitendo ili matokeo yake yaonekane kwa umma,” alisema.
Pia Dk Slaa alisema sehemu kubwa ya hotuba za mawaziri hao zililenga katika ‘tutafanya’, hali iliyoonyesha kuwa ni ahadi zilizotolewa miaka mingi pasipo utekelezaji.
Dk Slaa alisema mafanikio yalitajwa na mawaziri wa CCM kwenye mkutano huo, ni sehemu ndogo ya matokeo yaliyopaswa kuonekana, hasa kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
“Mafanikio wanayoyataja ni mfano wa punje tu, sehemu kubwa ya pato la nchi hii linaliwa na watu wachache,” alisema.
Dk Slaa alisema kama fedha zilizoibwa na mafisadi zingenusuriwa na kurejeshwa kwa ajili ya uboreshaji wa maendeleo na ustawi wa jamii, mafanikio yangepatikana zaidi ya yaliyotajwa na mawaziri wa serikali ya CCM.
Kwa upande wake, Mbowe alisema kauli iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Steven Wassira, kuhusu uhusiano wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na marehemu Elikaeli Mbowe (baba yake mzazi), ililenga kuupotosha umma.
“Mzee Mbowe alikuwa na uhusiano na Mwalimu Nyerere katika kutetea haki na kuingiza damu ya Utanzania ndani ya mioyo ya wananchi, sina haja ya kumjibu sana Wassira lakini ajue kwamba waliopo sasa ndani ya CCM wanaendeleza maslahi binafsi tu,” alisema.
Alithibitisha marehemu Mbowe kushiriki harakati zilizoongozwa na Mwalimu Nyerere, lakini akasema uhusiano wao ulilenga kuitumikia jamii na si kuiba na kupora rasilimali za umma.
Alitoa mfano kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho ni Anna Abdallah ambaye ni mke wa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na Mbunge wa zamani wa Lulindi, lakini ameshindwa kusaidia kero zinazowakabili wakulima wa korosho.

Ureno yaitoa jasho Ujerumani

  Ureno
Timu ya Ureno ilionyesha haikuwa na mchezo wa kusisimua
Bao la Mario Gomez ambalo lilifungwa kwa kichwa na katika dakika za mwishomwisho katika mechi ya pili Jumamosi dhidi ya Ureno liliiwezesha Ujerumani kuondoka na ushindi wa goli 1-0.
Tangu mwanzo ilionekana kwamba Ureno ilikuwa katika hali nzuri ya kuitatiza timu ya Joachim Loew katika mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Lviv.
Ujerumani ilionekana kumiliki mpira kwa muda mrefu, lakini haikupata nafasi za moja kwa moja za kupata mabao.
Hata hivyo katika kipindi cha pili, Gomez alifanikiwa kufunga, baada ya kuupokea mpira kutoka kwa Sami Khedira, na kuianzishia Ujerumani kampeni safi ya Euro 2012 kwa ushindi huo.
Ureno walionekana kuwa hafifu, na waliamka mara tu baada ya Ujerumani kufunga, lakini ikawa vigumu kusawazisha.
Pepe aligonga mwamba, na baadaye hayo pia yakampata Nani, na ilielekea kweli ushindi ulikuwa ni wa Ujerumani.

Denmark yaishangaza Uholanzi

 Uholanzi na Denmark
William Kvist wa Denmark na Wesley Sneijder wakishindania mpira
Bao la Michael Krohn-Dehli ambalo lilikuwa ndio goli la pekee katika mechi ya kwanza Jumamosi, na ambalo lilifungwa katika kipindi cha kwanza cha mchezo, liliwezesha Denmark kupata ushindi na kuishangaza Uholanzi, ambayo licha ya kupata nafasi nyingi, haikuweza kutumbiza chochote wavuni.
Krohn-Dehli aliweza kuwakwepa walinzi wawili wa Uholanzi na kutia mpira wavuni.
Licha ya Uholanzi kuumiliki mpira vyema, Arjen Robben na Robin van Persie walijivurugia nafasi nyingi za kuibuka washindi.
Robben alikaribia sana kufunga alipogonga mwamba, na Denmark iliponea chupuchupu dakika za mwishomwisho wakati Uholanzi ilidai kwamba Lars Jacobsen alikuwa ameunawa mpira katika lango.
Kocha wa Denmark, Morten Olsen, kabla ya mechi alikuwa amenukuliwa akisema kwamba Uholanzi ni timu bora zaidi kuishinda timu yake, na wengi watayafikiria matamshi hayo yalikuwa ni ya kupimana nguvu kiakili.
Kwa kipindi kirefu katika mechi hiyo ya kundi B katika uwanja wa Metalist, inaelekea kwamba maneno ya Morten Olsen yalikuwa sahihi, kwani timu yake ilionekana kulemewa.
Uholanzi ilionyesha kujipanga vyema, na mchezo stadi na wa kasi, ikiwa na ubunifu mkubwa, na mashambulizi ya mara kwa mara.
Van Persie, ambaye aliifungia klabu ya Arsenal ya England magoli 36 katika msimu uliopita, hakuweza kuiokoa Uholanzi.
Hata hivyo Denmark ilijitahidi vilivyo katika mechi hiyo, ikiongozwa na nahodha Daniel Agger.

Uganda 1 Senegal 1

Timu ya Taifa ya Uganda Cranes imejitahidi kuzima kitisho cha nyota wa Ligi kuu ya England waliomo kwenye Timu ya Teranga wa Senegal katika mchuano uliochezwa kwa kasi kwenye uwanja wa Mandela huko Nambole mjini Kampala.
Papiss Demba Cisse
Papiss Demba Cisse
Mabao ya Pappis Cisse na Godffrey Walusimbi yalitosha kuwaidhisha mashabiki wa Uganda Cranes nyumbani.
Bao la Senegal lilipatikana mnamo dakika 10 kabla ya kipenga cha mapumziko baada ya Ndoye Dane kuusuka mpira na kuwapita mabeki watatu wa Cranes upande wa kushoto na kutoa pasi kwa Papiss Demba Cisse aliyeuweka katika lango tupu kuipa Senegal matumaini.
Hadi mapumziko ni Senegal iliyohesabu bao 1-0 lakini Uganda Cranes ilirejea kipindi cha pili na nia ya kubadili mchezo.
Licha ya shinikizo kali zilizowaelekea wachezaji wa Simba wa Teranga Waganda walijitahidi hadi nusu saa baadaye ambapo Papa Sane alimuangusha Geoffrey Massa katika eneo la hatari na Refa kuonyesha alama ya tuta.
Hapa ndipo Godfrey Walusimbi alipojitokeza kuikoa Uganda Cranes na kumuelekeza kipa Sane upande mwingine na kuuchonga mpira upande wa pili.
Simba wa Teranga walicharuka lakini mashambulizi yao ya kushtukiza yalizimwa mnamo dakika za mwisho na mechi kumalizika kwa 1-1, hii ikiwa mechi ya pili katika kipindi cha wiki moja Uganda Cranes kumaliza mechi kwa sare ya 1-1 ambapo huko Angola walilazimisha matokeo kama hayo dhidi ya Angola.

Ajali Kenya, waziri Saitoti afariki

Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Abiria wote saba waliokuwa kwenye ndege hiyo wanaarifiwa kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.
Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong. Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo

Mafanikio ya Diamond ndani ya miezi sita, balaaaah!

 IKIWA ni mwezi wa sita ambapo kwa kawaida mwezi huu unaugawa mwaka , kwa binaadamu mwenye malengo huwa tayari anajua nini muelekeo wake na nini amevuna.

Kutokana  hilo  msanii, Nassib Abdul a.k.a Diamond ambaye tangu kuanza kwa mwaka huu amekuwa akiwika ndani na nje ya nchi, anazungumza kiundani katika kipindi hiki amefanikiwa kiasi gani.


Starehe:Hongera sana kwa kuugawa mwaka salama.

Diamond:Nashukuru sana kwani siku hizi kifo kipo mkononi.

Starehe:Tukiwa tunaugawa mwaka na wewe ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri mwaka huu labda siri ya mafanikio yako ni nini?

Diamond:Kiukweli siri ya mafanikio yangu ni kujituma kwa bidii lakini zaidi ni malengo ambayo hujiwekea kabla ya mwaka kuisha kwamba mwakani nitafanya hivi na hivi.

Starehe: Kwa maana hiyo unataka kusema mafanikio yako uliyatarajia?

Diamond:Kulingana na mipango  yangu na malengo niliyojiwekea mwaka jana ni kama nilikuwa nawaza kupata mafanikio ingawa kwa kiasi kikubwa nilitegema zaidi mashabiki watakavyonipokea bila kusahau nini nitawapa.

Starehe:Enhee....

Diamond:Hiyo ndio siri pekee pamoja na kutegemea mashabiki lakini pia nilisoma soko la muziki linataka nini si unajua sasa hivi Dunia ni kama kijiji,kinachoimbwa Marekani kinakuja huku kwetu kama upepo lakini kuna nchi jirani ambazo kwa kiasi fulani tabia zetu zinafanana, hivyo hata ujumbe uliopo kwenye tungo zetu unaendana japo sio sana.Kabla ya kutoa wimbo ili mashabiki waupende inabidi uangalie mambo kama hayo.

Starehe:Unaonaje ushindani wa muziki kwa majirani zetu, yaani Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda n.k

Diamond:Kwanza kabisa nakuhakikishia kwa nchi za Afrika Mashariki Tanzania tupo vizuri kimuziki na ndio maana tunakubalika nchi zote tano,nasema hivyo kwa kuwa wanamuziki ambao tunafanya vizuri hapa nyumbani tupo wengi tofauti na nchi nyingine kati ya hizo tano ambazo labda msanii anayetamba ni mmoja mmoja.Starehe:Mbona umejibu kwa kujiamini unaweza kunipa mfano hata mmoja kuthibitisha hilo?

Diamond:....Kicheko...mifano ipo mingi lakini mmojawapo ni kwamba hawezi kuja msanii kutoka kati ya nchi hizo akapata mashabiki wengi kutoka kwetu bila kushirikiana na wanamuziki wa hapa nyumbani, hiyo inaonyesha kuwa hawana uwezo kushinda sisi na ndio maana waandaji wamelitambua hilo na kuhakikisha akija mwanamuziki na wenyewe tunakuwepo ili kuwapa raha mashabiki wetu. Sisi tuna uwezo wa kwenda nchi nyingine na kupiga shoo bila kumshirikisha msanii kutoka nchi tuliyoenda.

Starehe:Hongera sana kwa niaba ya wanamuziki wenzako,lakini turudi kwako wewe binafsi ni shoo gani kali umepiga tangu kuanza kwa mwaka huu hadi kufikia sasa?

Diamond:Tabasamu pana....Kiukweli zipo mbili na nikitaja moja nitawapunja mashabiki wangu ambao kwa nia moja ama nyingine wananiunga mkono kila ninapofanya shoo.


Starehe:Mmh...ni zipi hizo Diamond?

Diamond:Nashukuru kwa kupata nafasi hii kwanza kabisa nawashukuru mashabiki wangu kwa jinsi walivyoniunga mkono katika shoo hizo,ambazo ni ile niliyopiga Mlimani

City ambayo niliipa jina la Diamond Are Forever,na ile niliyopiga Mbagala katika Ukumbi wa Dar Live kiukweli sitazisahau na ninasema ahsante sana mashabiki wangu.

Starehe:Bado hujatueleza vizuri kwa nini huwezi kuzisahau na unajivunia kuwa mwanamuziki kwa shoo hizo tangu mwaka huu uanze ?

Diamond:Huwezi amini kwenye shoo ya Mlimani City nilikusanya zaidi ya sh80mil za Tanzania na ya Mbagala nililipwa sh10mil bila utata wala longolongo yoyote.

Starehe:Zaidi ya kukusanya fedha nyingi nini kilikufurahisha na kujivunia.

Diamond:Sikufichi ni shoo ya Mbagala,kwa sababu ni shoo iliyokutanisha watu wa rika zote wakubwa, watoto,vijana na watu wa makamu walionifurahisha zaidi ni watoto kwa kuwa waliweza kunisubiri na hii ni faraja kwangu kwa kuwa nimeona ni kwa jinsi gani ninapendwa na kutoa burudani kwa watu wa rika zote nimefurahishwa sana na hilo.

Starehe:Kutokana na kiwango chako kupanda na hivi majuzi umepaform kwenye jumba la Big Brother ni wasanii Wangapi wa nje ambao wametaka kufanya kolabo na wewe.

Diamond:Hata kabla ya kwenda Big Brother ambayo na hiyo ni moja ya mafanikio kwangu,wasanii wengi wa nje ingawa sipendi kuwataja walikuwa wananiomba nifanye nao kolabo lakini kuna mambo yalinifanya niwe bize kidogo nikikaa vizuri kila kitu kitakuwa poa.
Diamond:Nikitoa kulinganisha na nchi nyingine kama nilivyokujibu mwanzo, muziki unakuwa huku changamoto ikiwa kubwa kwa wanamuziki wakongwe kwa kuwa kuna wanamuziki wanaibuka, ingawa hawadumu kwenye fani lakini akitoa nyimbo inakuwa juu sasa kama hujasimama imara lazima uyumbe.

Starehe:Ndio unataka kusemaje hasa kwa hao wanaoingia na kutoka na kwa nyinyi wakongwe.

Diamond:Wanaoingia na kutoka sina komenti kwa kuwa labda hawakujipanga, kazi inabaki kwa wakongwe kuhakikisha wanapambana na changamoto hii,kwani kutolewa nishai na mwanamuziki chipukizi ni aibu.

Starehe:Mashabiki wako wategemee nini mwezi huu ambapo tupo katikati ya mwaka 2012.

Diamond:Kwanza kabisa kabla ya yote wakae mkao wa kula kupokea video ya wimbo wa 'Lala salama' na nimpende nani,nasema ni kali narudia tena ni kali wakae mkao wa kuburudika roho ,mwili,akili na macho pia kwa kuona kitu kizuri.

Starehe:Pamoja na mafanikio uliyoyapata wewe binafsi lakini hali ya muziki unaionajeDiamond:Nikitoa kulinganisha na nchi nyingine kama nilivyokujibu mwanzo, muziki unakuwa huku changamoto ikiwa kubwa kwa wanamuziki wakongwe kwa kuwa kuna wanamuziki wanaibuka, ingawa hawadumu kwenye fani lakini akitoa nyimbo inakuwa juu sasa kama hujasimama imara lazima uyumbe.

Starehe:Ndio unataka kusemaje hasa kwa hao wanaoingia na kutoka na kwa nyinyi wakongwe.

Diamond:Wanaoingia na kutoka sina komenti kwa kuwa labda hawakujipanga, kazi inabaki kwa wakongwe kuhakikisha wanapambana na changamoto hii,kwani kutolewa nishai na mwanamuziki chipukizi ni aibu.

Starehe:Mashabiki wako wategemee nini mwezi huu ambapo tupo katikati ya mwaka 2012.

Diamond:Kwanza kabisa kabla ya yote wakae mkao wa kula kupokea video ya wimbo wa 'Lala salama' na nimpende nani,nasema ni kali narudia tena ni kali wakae mkao wa kuburudika roho ,mwili,akili na macho pia kwa kuona kitu kizuri.

Bob Makani afariki dunia

MWASISI wa Chadema na Mwanasheria mkongwe nchini Bob Makani, amefariki dunia usiku katika hospitali ya Aga khan, jijini Dar es Salaam.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, Makani alizidiwa ghafla saa 3: 00 usiku wa kuamkia leo na kukimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako alifariki dunia saa 4.15 usiku.

“Amekuwa anaumwa muda mrefu, mara kadhaa akipelekwa hospitali na baada ya muda anaruhusiwa, lakini hii ya sasa alikua nyumbani akazidiwa ghafla wakampeleka hospitali na ilipofika saa 4.15 wakasema amefariki,” alisema Zitto.

Zitto alisema kuwa, suala la wapi utakapozikwa Makani ambaye ni Katibu Mkuu wa Kwanza na Mwenyekiti wa pili wa Chadema, litajulikana baada ya kujadiliana na familia ya marehemu.

“Suala la wapi atazikwa kama ni Shinyanga ama Dar es Salaam, litajulikana baada ya kuzungumza na familia yake, kwa sasa tunashughulika kwanza na kuhifadhi mwili wa mzee wetu,” alisema Zitto.
Zitto alisema msiba wa utakuwa nyumbani kwa marehemu eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Kwa siku za hizi karibuni afya yake imekuwa ikizorota na kumfanya kuripotiwa kuanguka mara kwa mara alipokuwa akifanya shughuli zake.

Januari 17 mwaka huu katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema Regia Mtema, Makani alianguka muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu.

 Baada ya tukio hilo, alibebwa na kupelekwa pembeni ambako alipepewa kwa takriban dakika tano kisha kurejea katika hali yake ya kawaida na kurudi kwenye kiti chake

Alikuwa Katibu Makuu wa kwanza wa Chadema kati ya mwaka 1993 hadi 1998, alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 na amegombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa mara tatu kati ya mwaka 1995 na 2000 na mwaka 2005.

Kazi ambazo amewahi kuzifanya serikalini; alikuwa naibu mwanasheria mkuu wa serikali, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mwaka 1966 na elimu yake ana shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha Makarere nchini Uganda.

Ni mzaliwa wa Wilaya ya Kishapu, mkoani Shinyanga akitokea kwenye ukoo wa kichifu wa Makani.

Friday, June 8, 2012

Mashindano ya urembo nchini yatumike pia kukuza utamaduni wa lugha

TUSIKUBALI. Inafaa Watanzania tutambue kwamba lugha ni sehemu ya  utamaduni unaoweza kulitambulisha taifa letu nje ya mipaka yetu.
Ndiyo maaana kumekuwapo na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) linalosimamia na kuratibu mambo mbalimbali yanayohusiana na lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.
Ieleweke wazi kwamba chombo hiki kinafanya kazi ya umma na siyo kwa ajili ya wasomi peke yao kama wengi wanavyodhani.
Miaka ya hivi karibuni kumekuwapo na mwamko wa mashindano haya maarufu kama Miss Tanzania ambayo mwaka huu yanafahamika kama Redd’s Miss Tanzania ambayo kwa sasa yamejitanua zaidi katika ngazi ya vitongoji.
Mashindano hayo yanayowahusisha kinadada, yamekuwa na mvuto wa aina yake hasa kwa vijana kwa ujumla.
Siyo tu ni njia ya kujipatia kipato, pia wengine wameibuka kuwa maarufu katika jamii na kuwawezesha kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii pindi wanapoibuka kuwa washindi.
Mathalan, kampuni nyingi zimekuwa zikijitokeza katika kudhamini mashindano hayo, wakati nyingine zikidhamini mtu mmoja mmoja kulingana na shughuli ambazo wanazokubaliana katika kutangaza kampuni hizo.
Mashindano yanayofanyika kwa ngazi ya vitongoji, kama vile yale yaliyofanyika hivi karibuni kule Manyara, Ilemela (Mwanza), (Tabata, Ilala) na kwingineko yamekuwa yakitangazwa kupitia vyombo vya habari na kupokewa kwa mwitikio mkubwa na wapenzi wake.
Lakini, jambo la kujiuliza licha ya kuwapata washindi hao ipo wapi nafasi ya utamaduni wa Mtanzania ama Mswahili kupitia mashindano hayo hasa kuhusu lugha ya Kiswahili.
Kutokana na ukweli kwamba lugha ni sehemu ya utamaduni wetu, ipo haja ya washiriki wa mashindanohayo kutumia lugha yao ,Kiswahili wanapojieleza mbele ya watazamaji wao kuhusu maswali mbalimbali wanayoulizwa na majaji wao.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba sina uhakika iwapo washindi wote wanaoshinda katika mashindano ya dunia, lazima wawe wanafahamu lugha ya Kiingereza.
Japo ni suala la muhimu kwa washiriki hao kuwa na ujuzi wa kuzungumza lugha mbalimbali za kimataifa ambazo zinaweza kuwapa fursa ya kuwasiliana na watu wa mataifa mbalimbali, lakini wasisahau Kiswahili na hivyo kusaidia kukikuza.
Zipo jamii ambazo bado hazikubaliani kabisa na mashindano hayo kutokan na  kashfa  mbalimbali zinazotokana na  baadhi ya washiriki kuonyesha matendo mabaya katika jamii baada ya kupata umaarufu. Pia, baadhi ya mavazi ambayo yanavaliwa na washiriki hao  katika maonyesho yao.
Hata hivyo,  waandaaji wa mashindano hayo wanaweza kubadili mitazamo hiyo kwa kuyafanya mashindano hayo kama sehemu ya kukuza utamaduni wa Mtanzania , kwa kuipa nafasi lugha yao Kiswahili.
Mara nyingi washiriki hao huwa wanafundishwa  namna nzuri ya kuwasiliana na watazamaji  kwa ufundi wa hali ya juu.
Licha ya kuwa mashindano hayo hujikita katika kutangaza vivutio vya ndani vya utalii, lakini kuna maeneo mengi ya utamaduni ambao wanasahau kuyapa kipaumbele, kama vile utamaduni wa lugha na sanaa za asili za Kitanzania kama vile uchongaji na ususi.
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) nalo ni mdau mkubwa katika kuhimiza hili ili liweze kuwa na tija kwa Watanzania na kizazi kichajo.
Kuuenzi utamaduni wa Kiswahili vilevile ni kumuuenzi  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo kama vile yeye alivyokuwa mstari wa mbele katika kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini.
Aidha taasisi za vyuo vikuu nchini ziimarishe mifumo  yake kwa kutoa fursa kwa watu wengi kujifunza lugha ya Kiswahili kwa njia ya elimu na masafa kwa ngazi mbalimbali.
 Ni ukweli kwamba vyuo vikuu vya mataifa yaliyoendelea vimekuwa vikiendesha mfumo huo, ambao unawapa fursa watu wanaopenda kujifunza Kiswahili kujifunza lugha hii na kusoma vitabu vya Kiswahili vilivyoandikwa na Watanzania kisha kufanya mazoezi kwa njia ya mtandao wa kompyuta.
Njia hii ya kupata elimu inaweza kuwasaidia hata kina dada (washiriki wa urembo) ambao wanapenda kutumia Kiswahili fasaha kwenye mashindano hayo, kuwa na hamasa ya kujifunza kisha kujieleza kwa Kiswahili fasaha.
Hii, pia itasaidia wageni wanaotaka kujifunza Kiswahilli cha Tanzania kunufaika na fursa hizo za elimu masafa  na ninatumaini wanaweza kuwa chachu katika kukuza uchumi wa taifa kwa namna moja au nyingine kwa kuwa watakuwa wakichangia  huduma hiyo.
Kutokana na hoja hiyo, mdau wa Kiswahili Thomas Athanas kupitia maoni ya mtandaoni anasema kwamba, kuhusu washiriki wa Miss Tanzania, waandaaji ndiyo huwa na makosa ya kuweka majaji wa taasisi nyeti kutoka nje na ambao hawatumii Kiswahili kila mara.

Kiasi kwamba endapo mrembo wetu atazungumza Kiswahili itakuwa ni vigumu kwa  jaji huyo kumpatia alama za ushindi.Anashauri kwamba ni vyema majaji wengi wakawa wazalendo.

Naye Profesa mstaafu wa masuala ya historia,Pete M. Mhunzi aliyeko Marekani anasema kwamba ni muhimu sana vijana Watanzania wawe gwiji wa lugha zote mbili pamoja  na lugha nyingine za dunia.
Lakini, kuchanganya lugha mbili kila moja ikiwa na nadharia tofauti, sarufi tofauti, historia tofauti, matokeo yake ni kutojua vizuri lugha yoyote.

Hivyo, waandaaji hao  waige mfano wa Mwalimu Nyerere kwani ni taa kwa wapenzi wote wa lugha ya Kiswahili na wanaopenda utamaduni wa Kitanzania au Kiafrika kwa jumla, kwani hakusisitiza kwa mdomo tu bali alisimamia kile alichokisema kwa vitendo.

Ifike mahali Watanzania tuwe wazalendo pia hata kwa lugha yetu,  kwani matunda haya tunayoyapata leo hii katika Kiswahili ni kutokana na mwasisi wa taifa hili kuona umuhimu wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya umoja wetu.

HUWEZI KUJIUNGA FREEMASON KWENYE MTANDAO

FAKE MASONRY
All links on this website will take you to information about Regular Freemasonry.
As a cautionary note, there are a few websites on the internet that offer membership in the fraternity of Freemasonry where they provide an online form and ask you to send in a payment, credit card information, etc., along with your contact information as a method to become a Free Mason.
BE AWARE!
The Freemason fraternity does not offer online membership. You cannot join Freemasonry via the internet.
All men interested in becoming a Freemason must contact a lodge (or a Grand Lodge, for direction in how to find a lodge near where they live).
As you can see from reading the above information of how to go about becoming a Freemason, it is a worthwhile process that takes time.
Masonic-Lodge-of-Education.com simply provides Masonic information about how you may properly contact the fraternity regarding membership.
False information about Freemasonry has abounded for centuries.
With the inception of the internet, and its ability to provide "instant" information to everyone, please be aware that there are websites on the internet which provide anti-Masonic rhetoric, conspiracy theories, and other malicious mis-information to the unaware and uninformed about how to become a Freemason.
Fortunately, however, there are many, many more Masonic websites built by members of the fraternity that are highly informative and which do an excellent job of providing truthful information, which does justice to the craft.
As more and more people learn about Freemasonry's true beliefs and ideals, this mis-information will soon become a thing of the past and fade away to its rightful place in the scrap heap